Mwanangu amenifanya kuwa mama bora zaidi - Nadia Mukami

"Mungu alijua nakuhitaji sana mwanangu @haseebkai! Nampenda huyu mtoto sana.

Muhtasari

• "Mungu alijua nakuhitaji sana mwanangu @haseebkai! Nampenda huyu mtoto sana.

• Amenifanya kuwa mtu bora maishani ♥️," Nadia alisema.

Nadia Mukami
Image: Nadia Mukami Instagram

Mwanamuziki wa Kenya, Nadia Mukami amesema jinsi mwanawe Haseeb Kai amemfanya kuwa mtu bora zaidi ya alivyokuwa kabla ya kumleta duniani.

Kwenye Instagram, alipakia video akiwa amembeba mwanawe kifuani huku wimbo wake wa 'Zawadi' ukiimba kwa umbali.

"Mungu alijua nakuhitaji sana mwanangu @haseebkai! Nampenda huyu mtoto sana. Amenifanya kuwa mtu bora maishani ♥️," Nadia alisema.

Mama huyo wa mtoto mmoja amekuwa akifurahia mwanawe kufikisha miezi minane tangu kuzaliwa.

Hata hivyo, licha ya mama huyo kupenda matukio yake ya kuwa mama, alisema kuwa hataki kupata mtoto mwingine hivi karibuni.

Hii ni baada ya kuulizwa kwenye Instagram iwapo anapanga kumleta mtoto mwingine duniani hivi karibuni.

"Tumtarajie mtoto wa pili hivi karibuni?" shabiki wake aliuliza.

Nadia alisema kuwa sasa hivi hana mipango ya kupata mtoto mwingine na kuwa anapanga kupata mtoto mwingine tena baada ya miaka mitano.

"Labda baada ya miaka mitano, sitaki saa hii! Eh ni kujitolea pakubwa sana," Mukami alisema.

Zaidi ya hayo, mpenzi huyo wa Arrow Boy alisema jinsi mpenzi wake humsaidia katika malezi.

Mukami alimwandikia mpenzi wake Arrow Boy ujumbe huku akimsherehekea siku ya wanaume duniani.

Kwenye Instagram Mukami alipakia video akimshukuru mwanamuziki huyo kwa kuwa baba mzuri kwa mtoto wao.

"Kwa baba ya mtoto wangu almaarufu mpenzi wangu wa maisha ambaye hunisaidia kumlea mtoto wetu, Kai 22/7 haswa asubui kwa kuwa mimi si mtu wa kuamka mapema kabisa !! Asante," Nadia aliandika.