Fahamu alichoambiwa Harmonize baada ya kuimba wimbo wa Diamond stejini Eldoret

Msanii huyo alipakia klipu kwenye Instagram yake akiimba na umati wimbo wa Iyo ambao Diamond aliwashirikisha wasanii kadhaa kutoka Afrika ya kusini.

Muhtasari

• Harmonize alikuwa mjini Eldoret nchini Kenya wikendi iliyopita ambapo alikuwa anachachisha umati akitumia kionjo cha wimbo wa Diamond – Iyo.

Harmonzie, Diamond Platnumz
Harmonzie, Diamond Platnumz
Image: Instagram

Msanii Harmonize amejipata pabaya baada ya kutumia kionjo cha wimbo wa hasidi wake katika muziki, Diamond Platnumz.

Harmonize alikuwa mjini Eldoret nchini Kenya wikendi iliyopita ambapo alikuwa anachachisha umati akitumia kionjo cha wimbo wa Diamond – Iyo.

Watu kwenye mitandao ya kijamii mashabiki wa wasanii hao wawili ambao hawaonani jicho kwa jicho walimshambulia vikali kwa kumchukia Diamond lakini kuendelea kutumia baadhi ya ngoma zake kuchagiza shoo zake.

“Konde we wanna party..” Harmonize aliimba wimbo huo kwa sehemu huku mashabiki waliojaa kwenye ukumbi Eldoret wakiimba na yeye kwa kuradidi.

“Hiki kipande mbona kama cha Simba, halafu unajifanya umemchukia?” mmoja aliuliza.

“Kumbe bado unamsikiliza Simba faraghani lakini hadharani unafanya kama anakuchefua vile.. wewe mnafiki sana aisee,” mwingine alimkoromea.

Harmonize alifanya shoo hiyo siku chache tu baada ya uvumi kusambaa mitandaoni kuwa ameachana na mpenzi wake wa muda mrefu Kajala Masanja.

Japo msanii huyo hajafichua wazi ukweli uliopo kweney uvumi huo, Kajala kwa upande wake aliweka wazi kuwa ameamua kuvunja uhusiano wake na kusema ashasamehe kila kitu na kusonga mbele.

Watu wamekuwa wakimpa shinikizo kurudisha magari ambayo Harmonize alimpa kama zawadi wakati anambembeleza kumrudia, huku wengine pia wakimpongeza kwa kukwama na magari hayo kwa kile wanasema kuwa hakutumika bure na magari hayo yanafaa kuwa kama faraja yake baada ya kutumiwa na Harmonize.

Gari arudishi mnamaanisha alitumika bure na mbwembwe za Nyadundo zile atoke kappa? Hapana” H-Baba alisema.

Baba Levo na Mwijaku wamekuwa mstari wa mbele kumshinikiza Kajala kurudisha magari ya Harmonize huku wakimtetea Harmonize kuwa alifanya uamuzi mzuri wa kumuacha mwanamke huyo ambaye kwa maneno yao walimtaja kama tapeli.