Shukuru Mungu safari hii hukuchora tattoo - Mwijaku kwa Kajala baada ya kuachana na Harmonize

Kajala alldhibitisha kuachana na Harmonize siku mbili zilizopita akisema anajuta kurudiana naye mwanzo.

Muhtasari

• Katika mapenzi yao ya awali kabla ya kuachana mwaka jana, wawili hao kila mmoja alikuwa na tattoo ya mwenzake.

Mwijaku ,Harmonize, Kajala
Mwijaku ,Harmonize, Kajala

Mwijaku amekuwa mtu wa hivi karibuni kuzungumzia sekeseke za kuachana kwa Harmonize na mchumba wake Kajala Masanja.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mwijaku alipakia picha ya mwigizaji huyo mkongwe na kumtaka amshukuru Mungu kwani kuachana kwake na Harmonize ni kama kujipatia uhuru kutoka kwa bepari.

Mwijaku pia alimwambia kuwa anafaa kuwa mwenye fadhila kwa Mungu kwani amemuacha Harmonize safari hii kabla ya kuchora tattoo yake kama ambavyo alikuwa amefanya awali mwaka jana walipoachana.

Mwaka 2021, Kajala kabla ya kuachana na Harmonize kwa mara ya kwanza, alikuwa na Tattoo ya Harmonize, wakati pia msanii huyo naye alikuwa amemchora Kajala mwilini mwake, lakini safari hii hawakuwa wamefikiwa hatua hiyo.

“Mshukuru Mungu safari hii hauja chora Tatooioo ..!” Mwijaku alimwambia Kajala.

Mwijaku pia kama kawaida yake hakukosa kumchokoza Diamond Platnumz kwa kupakia picha ya Zuchu na kusema kuwa ipo siku pia atamuacha Diamond na hali itakuwa vibaya mno kwa bosi huyo wa WCB Wasafi.

“Ikitokea na wewe siku una muacha MWAMBINO sijui itakuaje..! Nadhani siku hiyo asipo kunywa klorokwini sijui maana anavo vimba mmh . Siku Moja NDIYO. Itafika tu hatuwezi kuipukaaa,” alisema.

Kwa upande wa Harmonize, Mwijaku alimshauri kutoingiwa na wasiwasi tena na mapenzi bali kuchukuwa muda wake kufanya mazoezi na kujinenepea mwenyewe. Alimtaka mambo ya mapenzi amuachie yeye tu kwa sababu ndiye mwenye kuyamudu.

“Kilichobakia jinenepeee tu mzee mwenzangu . Mapenzi niachie mimi ndie nayamudu DC,” Mwijaku alishambulia Harmonize.

Za ndani zinasema Harmonize ameshamwagwa na kumiminwa na Kajala baada ya kile ambacho hakijadhibitishwa lakini wambea wanasema msanii huyo alimpachika mchepuko mimba, wengine wakisema mhusika wa mimba ni Anjella.

Harmonize mpaka sasa hajazungumza azi iwapo ni kweli ameachwa na Kajala lakini kwa upande wake, mwanamke huyo alidhibitisha kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alisema kuwa anajutia sana hadi kujibeza kuwa anastahili kuchekwa kwa mamuzi yake ya kumrudia Harmonize.

Harmonize na Kajala walikuwa wanatarajiwa kufunga ndoa haswa baada ya tukio lile la mwezi Juni ambapo walivishana pete za uchumba.