Simuachi-Karen hatimaye azungumza baada ya kusababisha drama kwenye tamasha ya Samidoh

Kwenye video hiyo, Samidoh ameketi eneo lake lakini ghafla bin vuu Karen anaamua kuketi kwenye mapaja yake.

Muhtasari
  • Huku akizungumzia suala hilo, Karen amesema kwamba alikuwa amelewa, na kwamba ameacha pombe
KAREN NYAMU
Image: HISANI

Seneta Karen Nyamu kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook amezungumza na kuweka mambo bayana baada ya kuvuma mitandaoni.

Karen alivuma baada ya video yake na mkewe Samidoh kutaka kupigana kwenye tamasha.

Huku akizungumzia suala hilo, Karen amesema kwamba alikuwa amelewa, na kwamba ameacha pombe.

Pia aliweka wazi kwamba hakujua kwamba lazima mtu awe na leseni ili apande jukwaani.

"Nimeamka nikapata nimevuma mitandaoni,pombe ni mbaya,mwaka wa 2023 sitaki drama,lakini nimeacha pombe, simuachi,"Karen Aliongea.

Katika video ambayo inasambaa mtandaoni, kisanga kinaonekana kuzuka wakati mmoja baada ya Karen kuamua kukaa naye eneo la watu mashuhuri.

Kwenye video hiyo, Samidoh ameketi eneo lake lakini ghafla bin vuu Karen anaamua kuketi kwenye mapaja yake. 

Inabidi Samidoh ajitoa lakini sekunde hazipiti kabla ya mkewe, Edday, pia kumshika mashati na kulazimisha walinzi kuingilia kati.

Karen aliondolewa kutoka steji na walinzi hao katika kisa hicho ambacho kimezua mdahalo mkubwa mtandaoni.

Wanamtandao wanakosoa mwanasiasa huyo wakisema anajaribu kuleta machungu kwa mke wa Samidoh.