Wewe ndio zawadi bora ya Krismasi Mungu alinipa - Mungai Eve amsifia mpenziwe Trevor

Mungai alisema anatumai kufurahia misimu yote ya krismasi pamoja na Trevor.

Muhtasari

• Wapenzi hao wanashirikiana katika kufanya kazi ya ukuzaji maudhui kwenye mtandao wa YouTube.

Mungai Eve na mchumba wake
Mungai Eve na mchumba wake
Image: Instagram

Mwanablogu wa YouTube Mungai Eve alisherehekea siku kuu ya Krismasi kwa njia ya kipekee na mpenzi wake muongozaji Trevor.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mungai Eve alipakia rundo la picha za wakiwa pamoja katika mazingira yaliyoonekana kuwa karibu na shamba la migomba ya ndizi na kumwambia mpenzi wake kuwa hakuhitaji zawadi yoyote ya Krismasi kwani yeye ni zawadi tosha.

Mungai Eve alizidi kumwaga yaliyo moyoni mwake kwa Trevor akimwambia kuwa ombi lake kila siku ni lile moja tu na kudumu pamoja kimapenzi ili kuwajibu wale wanaosema kuwa huenda mapenzi yao hayataenda popote.

“Wewe ni zawadi bora zaidi ya Krismasi ambayo Mungu alinitumia! Hebu tutumie Krismasi isiyo na kikomo pamoja mpenzi wangu Director Trevor,” Mungai Eve aliandika.

Wapenzi hao wawili ambao wanashirikiana kwa kufanya kazi ya ukuzaji maudhui pamoja kwa muda mrefu wamekuwa wakiwekwa chini ya shinikizo na mashemeji wa mitandaoni katika kile wanasema ni kuchelewa kuwapa taarifa za mtoto.

Mungai Eve naye kwa vile ana mdomo hajakuwa mvivu wa kujibu mipigo kwa wale wanaomwekea shinikizo la kupata mtoto.

Aliwajibu kuwa wanaomtaka kupata mtoto si wao wa kumpangia maisha yake kwani yeye na mpenzi wake ni watu wazima na wanajua malengo yao ya kimaisha huku pia akidokeza kuwa muda mwafaka ukifika watapata mtoto.

Wiki kadhaa alipolazwa hospitalini, Mungai Eve alifanya video ambayo aliwatania watu kutaka kuotea iwapo ugonjwa wake ulikuwa ni kutokana na mimba.