Amber Ray ataja sababu ya kumchukia Amira, "Aliniita kahaba mvunja ndoa!"

Alisema kuwa Amira alikuwa anamuita changudoa wa kuvuruga ndoa za watu lakini naye akafukuzwa kwa sababu hiyo hiyo.

Muhtasari

• Amber Ray alionekana kujibu kuwa ni kejeli zake ni njia moja ya kulipa kisasi katika yale mabaya ambayo Amira alikuwa anamhusisha nayo.

Amber Ray asema kwa nini hampendi Amira
Amber Ray asema kwa nini hampendi Amira
Image: INSTgram

Mwanasosholaiti Amber Ray hatimaye amefichua sababu yake ya kuendeleza michambo yake dhidi ya aliyekuwa mke mwenza, Amira katika ndoa ya wake wawili kwa mfanyibiashara Jimal Rohosafi.

Kwa muda mrefu tangu wawili hao kukorofisha kwa sababu ya Rohosafi na mwisho wa siku wote wawili kusalimu amri katika ndoa hiyo, wamekuwa wakionekana kutupiana cheche za maneno ya kebehi mitandaoni kwa njia fiche jambo ambao limewafanya wengi kuamini kuwa huenda uadui wao ni wa paka na panya – kutopikika kwenye chungu kimoja.

Wakati wa kipindi cha maswali na majibu na mashabiki wake Instagram, mmoja alitaka kujua ni kwa nini muda wote Amber Ray anaandika jumbe mbaya mbaya kuhusu aliyekuwa mke mwenza Amira, na hakina Amber Ray hakuwa bahili wa maelezo.

Alisimulia kuwa Amira akiwa kama mke mkubwa alikuwa anamuona Amber Ray kama nyumba ndogo ambaye lengo lake lilikuwa ni kuvuruga ndoa yake. Pia alisema Amira alikuwa aanmchukulia kama changudoa ambaye kazi yake ilikuwa kunyakua wanaume wa wqatu.

Baadae yeye sasa amejinyakulia mchumba Kennedy Rapudo na hilo ndilo limezidisha chumvi kwenye msosi wa Amira kwani Amber Ray hakosi kumtupia kejeli kuwa yeye bado hajapata mume na yule aliyekuwa akidhani ni cangudoa wa kuharibu ndoa za watu tayari ameshavishwa pete ya uchumba akisubiria ndoa.

“Kusema kweli mimi simchukii (Amira) lakini kusema kweli alikuwa ananizungumzia kwa mabaya hapa mitandaoni. Unaua maisha wakati mwingine ni kitu cha kuchekesha sana, na siwezi jizuia, acha tu nicheke. Ushinde ukiita mtu changudoa na mwisho wa siku wewe ndio ufukuzwe kwa ukahaba… nyinyi wote mnaeza endelea kunihukumu lakini siwezi jizuia kucheka tafadhali,” Amber Ray alisema.

Hivi majuzi, Amber Ray alivujisha mazungumzo ya mama yake katika kikundi cha WhatsApp cha familia yao akisujudu kuwa hii ndio Krismasi anasherehekea na wanawe wote wakiwa na wachumba wao.

Kennedy Rapudo alimvisha pete ya uchumba Amber Ray wiki kadhaa zilizopita katika sehemu moja ya burudani jijini Dubai.