Nashukuru Mungu hakuna mtu singo kwa familia yangu - Mamake Amber Ray

Mamake mwanasosholaiti huyo alikuwa akiwajulia hali wanawe kwenye kikundi cha WhatsApp.

Muhtasari

• Wiki chache zilizopita, Amber Ray alivishwa pete ya uchumba na mpenzi wake Kennedy Rapudo wakiwa ziarani Dubai.

• Wawili hao walikuwa wameachana kwa muda kisha wakarudiana kwa kishindo kikubwa kilichohitimishwa na kuvishana pete za uchumba.

Kennedy Rapudo na mpenzi wake Amber Ray
Kennedy Rapudo na mpenzi wake Amber Ray
Image: Instagram

Mamake mwanasosholaiti Amber Ray ni mtu mwenye furaha baada ya mabinti zake wote kufanikiwa kujitilia kibindoni ndoa.

Amber Ray alifichua mazungumzo ya mamake kwa wanafamilia wake kwenye mtandao wa WhatsApp ambapo alianza kuwajulia hali huku akimwaya furaha yake kuwa ana fahari kubwa kwa wanawe kwa sababu safari hii hakuna aliye bila mchumba – Singo.

Katika kile ambacho kilionekana kama mkutano wa kifamilia, ujumbe wa mamake Amber Ray unadhihirisha furaah iliyoko moyoni mwake ambapo alisema kuwa ni furaha kubwa kuzungumza na wanawe wote kupitia kikundi cha WhatsApp akiwa anajua fika kuwa wote ni kila mtu na ndoa yake safi kama pamba.

“Hamjambo watu wa familia yangu, krismasi mmepanga aje? Nashukuru Mungu safari hii hakuna mtu singo kwa familia yangu. Mungu ni mkubwa!” mama mtu alisema kwa furaha.

Ikumbukwe katika tamaduni za miaka na mikaka, familia nyingi kote duniani zimekuwa zikikutana na kufurahia pamoja wakati wa msimu wa sikukuu za krismasi.

Amber Ray hivi majuzi alivishwa pete ya uchumba na mpenzi wake wa muda mchache mjasiriamali Kennedy Rapudo katika mandarin ya kutamanisha ambapo baadae walifanya ziara za kama fungate vile katika visiwa vya Zanzibari.

Rapudo, alimposa mama huyo mrembo wa mtoto mmoja mapema mwezi wa Novemba, alipokuwa akifurahia chakula cha jioni huko Dubai, akimuacha akiwa ameduwaa. Katika video iliyoshirikiwa kwenye ukurasa wa Instagram wake Amber, wawili hao walikuwa wakifurahia dina pamoja jioni, na alionekana mrembo akiwa amevalia rinda refu jekundu. Mahabubu wake baadaye alipiga goti moja kuomba uchumba naye akiwa ameshikilia pete.