Bien amtetea mkewe kwa kumfukuza mwanadada aliyejaribu kutingika ukumbini

Katika video, mwanadada alionekana akitingika nyuma ya Bien kabla ya mkewe Chiki Kuruka kufika na kumfukuza.

Muhtasari

• "Kwa hiyo msiangalie kitu kama kile muone kama mke wangu anakuwa na wivu, ni kazi yake." - Bien alisema.

Bien amtetea Mkewe Chiki Kuruka kwa kumfukza mwanamke ukumbini
Bien amtetea Mkewe Chiki Kuruka kwa kumfukza mwanamke ukumbini
Image: Instagram

Msanii Bien Aime Baraza wa kikundi cha Sauti Sol amemtetea vikali mkewe Chiki Kuruka baada ya kuonekana kumsukuma mwanamke aliyejaribu kumtingishia makalio mumewe akiwa anatumbuiza kwenye ukumbi.

Wikendi iliyopita, Bien alikuwa anatumbuiza katika tafrija moja iliyoandaliwa na kampuni ya pombe.

Akiwa ukumbini, mwanamke mmoja ambaye hajatambulika kwa jina alipanda jukwaani na kuanza kucheza densi nyuma ya mgongo wake kwa mwenendo wa kimahaba.

Jambo hilo kama halikumfurahisha mkewe Bien, Chiki Kuruka ambaye aliwahi pale kwa upesi na kumsukuma mwanamke huko kutoka ukumbini na kutokaribia mumewe.

Wengi walihisi kwamba Chiki alikuwa anaonesha wivu wa mapenzi ambao haswa watu wengi katika mahaba huonesha, kutokana mtu wa jinsia nyingine kumkaribia mpenzi wake iwe hadharani au faraghani.

Lakini Bien ametetea kitendo kile akisema kuwa wote walikuwa kazini, na mkewe ndiye meneja wa kazi zake za kimuziki kwa hiyo alikuwa na kila sababu ya kumfukuza mwanadada yule, wala halina kitu chochote kuhusiana na wivu wa mapenzi.

“Chiki alikuja pale kufanya kazi yake, ni meneja wako na alichokifanya ni kutekeleza wajibu wake kama meneja. Kwa hiyo msiangalie kitu kama kile muone kama mke wangu anakuwa na wivu, ni kazi yake. Anafaa kuhakikisha kwamba kabla nipande ukumbini, niko vizuri kwa namna zote na usalama wangu pia,” Bien alisema.

Bien alisema kuwa yule mwanadada aliyekuwa akimtingishia maungo mgongoni mwake alikuwa anamletea usumbufu na ndio maana mkewe Chiki Kuruka kwa kushirikiana na walinzi walifika haraka na kumtoa kabla ya kuvuta fikira zake kutoka kwa kutumbuiza hadi kwa kuanza kuangalia jinsia alikuwa anatingisha kile alichobarikiwa nacho.

“Hakuan mtu alikosea mwingine ukiangalia hata yule mwanadada alikuwa amelewa kidogo anacheza densi anafanya mambo yake, lakini pia mimi na Chiki tulikuwa kazini kwa hiyo hakuna aliyekosea mwingine hata hivyo,” Bien alisema.