Willy Paul amfichua Zuena wake

Nandy ndiye Zuwena wake Willy Paul.

Muhtasari

•Msanii Willy Paul alidai kuwa alimlipa Zuwena wake shilingi milioni 2 ili kucheza kama vixen kwenye video yake.

Msanii Willy Paul almaarufu Pozee  alimfichua Zuwena wake aliyedai kuwa angewatambulisha kwa mashabiki wake karibuni.

Zuwena wake Willy Paul  haikuwapata mashabiki kwa mshtuko kwa sababu huyo Zuwena ni msanii wa Tanzania, Nandy.

Willy Paul alisema kwenye mtandao wa Instagram kuwa alibaki kapera kwa ajili ya Nandy na kuonekana kuwa wako kwenye harakati  kutengeneza kibao na na Nandy huu wakisema atapeana habari zaidi.

"Mshangao kwenu,ndiye huyu hapa, Nandy, nimekuwa kapera  kwa ajili ya huyu,habari zaidi inakuja,"

Msanii Willy Paul alidai kuwa alimlipa Zuena wake shilingi milioni 2 ili kucheza kama vixen kwenye video yake.

Willy Paul aliwakashifu wale waliomsuta wakisema kuwa alinakili wazo wa wimbo wake msanii wa Tanzania Diamond Platinumz aliyetoa kibao cha Zuwena mwezi mmoja uliopita.Pozze alisema aliwakejeli kwa kusema shilingi milioni 2 alizomlipa zilikuwa za Kenya na si Tanzania.

"Baada ya kusikiliza kisa cha Zuena ilibidi nimweke Zuena huyo huyo kwenye wimbo, sioni shida yoyote ,elewa kwa upole ,si jambo zito"alisema mtanadaoni.

Willy Paul pia alidai pia kuwa Zuwena aliyemtumia kama vixen ni mrembo mara hamsini zaidi ya ule wa wimbo asili wa Zuwena wake Diamond.