Rayvanny adokeza kumshirikisha Fahyma kwenye kibao kingine

Rayvanny alimsifia mzazi huyo mwenzake kwa urembo wake.

Muhtasari

•Rayavanny alisema kwamba kwa jinsi Fahyvanny alivyo mrembo sana ,kibao alichomshirikisha hapo awali hakitoshi hivyo itabidi kurekodi naye video yake inayofuata.

Rayvanny na Fahyvanny wakioneshana mahaba mazito baharini kwenye boti.
Rayvanny na Fahyvanny wakioneshana mahaba mazito baharini kwenye boti.
Image: Screengrab//Instagram

Staa wa Bongo Raymond Shaban Mwakyusa almaarufu Rayvanny amedokeza kuwa ana mpango wa kumshirikisha mpenziwe Fahyma kwenye wimbo mwingine.

Katika ukurasa wake wa Instagram, mwimbaji huyo alisema kwamba kwa jinsi Fahyvanny alivyo mrembo sana ,kibao alichomshirikisha hapo awali hakitoshi hivyo itabidi kurekodi naye video yake inayofuata.

"Kwa jinsi alivyo chombo, nashoot naye video yangu inayofuata, Forever haitoshi," alisema Rayvanny huku akimweleza mwelekezaji wake kuhusu mpango huo wake.

Kwenye posti hiyo aliyoipakia, Fahyma alimjibu Rayvanny akionyesha upendo.

"Mume wangu," alisema Fahyma.

Vanny Boy pia alieleza furaha yake baada ya wimbo mpya huo kutazwa sana kwenye mtandao wa Instagram.

Rayvanny alimshirikisha Fayhma katika kibao cha Forever huku akiahidi kumpenda Fahyvanny daima kwenye wimbo huo.

Rayvanny alionekana kurudiana na ex huyo wake kwenye wimbo wao wa Forever.Wameonekana pia wakiwa pamoja na wamefichua mipango ya za kufanya miradi pamoja.

Hata hivyo, hii si mara ya kwanza wawili hao kudokeza kuwa wamerudiana, japo ndio kama mara ya kwanza kabisa wanaibua mahaba yao hadharani, takribani miaka minne na miezi kadhaa baada ya kuachana

Rayvanny alimmiminia sifa mpenzi wake kwa  urembo wake asilia na kusema kuwa atakuwa kando yake kila wakati.Rayvanny na Fahyvanny waliwachana mwaka wa 2020 kisha Vanny akachumbiana na mwana wa Fridah Kajala, Paula Kajala.