Video: Msanii ajirekodi akila mende baada ya kuchora tattoo ya msalaba kwenye ulimi

Msanii huyo wikendi iliyopita alichorwa tattoo ya msalaba mweusi kwenye ulimi wake kabla ya Jumatano kujirekodi akila mende.

Muhtasari

• Lil mwenye umri wa miaka 27 kwa sasa anatamba na kibao cha "I just wanna rock".

• Mitandaoni, Lil hujitamulisha kama "wao" utambulisho unaotumiwa na watu wa LGBTQ.

Rapa wa Marekani Lil Uzi Vert ajirekodi akila mende
Rapa wa Marekani Lil Uzi Vert ajirekodi akila mende
Image: Instagram

Msanii wa rap kutoka nchini Marekani, Lil Uzi Vert amegonga vichwa vya habari mitandaoni baada ya kupakia video kwenye ukurasa wake wa Instagram akifurahia kula mende mkubwa.

Katika video hiyo ya sekunde 24, Lil anaonekana akichukua mende huyo mkubwa aliyekuwa amedungwa kwenye kijiti kama mishikaki na kutia mdomoni kabla ya kutafuta akiwa na tabasamu pana usoni.

Msanii huyo mwenye utata mwingi amekuwa akishtumiwa kuwa katika jamii ya kishetani kutokana na michoro ya tattooes zisizoeleweka kwenye mwili wake.

Video hiyo ambayo sasa ndio gumzo kwenye mtandao wa Tweeter inamuonesha Lil akila Mende na inasemekana kwamba alikuwa Thailand.

Lil anaendelea kutamba na ngoma ya ‘I just Wanna vibe’ ameshtumiwa na mashabiki ambao walihisi kwenye Twitter kwamba wamempoteza, baadhi wakimtaka kujifaidisha kutokana na kutrend kwake kwa kuwekeza nguvu nyingi kutoa kazi za kimuziki kuliko kufanya vimbwanga kama hivyo.

Jumatano pia TMZ waliripoti kuwa rapa huyo alichora tattoo ya msalaba kwenye kichwa chake pamoja na nyingine kwenye ulimi wake.

“Lil Uzi Vert amekuwa akijichora tattoo hivi majuzi, akionyesha kipande kikubwa kipya kwenye paji la uso wake na msalaba kwenye ulimi wake ... na kuwaacha mashabiki wakishangaa. Rapa huyo wa "Just Wanna Rock" alitembelea Studio ya Ganga Tattoo huko L.A. wikendi iliyopita, na kuibuka na Msalaba mweusi wa Saint Peter wenye rangi kwenye ulimi wake,” TMZ waliripoti.

Kwenye mitandao yake ya kijamii, Lil hujitambulisha kama "wao" kijinsia, utambulisho ambao aghalabu hutumiwa na watu wa jumuiya ya LGBTQ,