Hapatikani!Mwanawe Akothee amtambulisha mpenzi wake kwa mashabiki

Mashabiki wameenda mbali zaidi kumpongeza kwa hatua ya ujasiri ya kumtakia kila la kheri maishani kwa kupata mpenzi wake mpendwa.

Muhtasari
  • Fancy Makadia amekuwa akisoma na kuishi nje ya nchi ambapo ana uwezo mkubwa katika lugha ya Kifaransa miongoni mwa maeneo mengine ya masomo.
FANCY MAKADIA NA MPENZIWE
Image: FANCY MAKADIA/FACEBOOK

Fancy Makadia, bintiye Akothee ​​ambaye ni mtoto wa tatu kuzaliwa katika familia ya watoto watano hatimaye amedhihirisha kwamba amepata mpenzi wake na hayuko sokoni.

Leo, ameingia mtandaoni kueleza jinsi mwanamume huyo anavyomuunga mkono na jinsi alivyorahisisha maisha yake, jambo ambalo limewafanya mashabiki wake wengi kujiuliza ni nini kimetokea kwa wanaume hao wa Kenya kwa vile mwanaume huyo ana asili ya kizungu.

Fancy Makadia amekuwa akisoma na kuishi nje ya nchi ambapo ana uwezo mkubwa katika lugha ya Kifaransa miongoni mwa maeneo mengine ya masomo.

Fancy huku akimtambulisha mpenziwe mitandao alimnakilia ujumbe maalum huku akimshukuru kwa kumpa ujasiri ambao umemwezesha kushinda chngamoto za maisha.

"Halo wewe, Hakika nimebarikiwa kuwa na wewe kama sehemu ya maisha yangu. Asante kwa kuwa mpenzi wangu, rafiki yangu, na msiri. Upendo wako umenipa ujasiri na ujasiri wa kuushinda ulimwengu huu. Ninakushukuru kwa kunifanya kuwa mtu bora zaidi. Ungeweza kuwa na mtu yeyote katika ulimwengu huu, lakini ulinichagua mimi. Asante. Nakupenda OC (Osiep Chunya)"Aliandika Makadia.

Image: FANCY MAKADIA/FACEBOOK

Mashabiki wameenda mbali zaidi kumpongeza kwa hatua ya ujasiri ya kumtakia kila la kheri maishani kwa kupata mpenzi wake mpendwa.