Harmonize humpigia Esma simu na kumpa Mama Dangote kuongea naye - mapya yaibuka

"Harmonize hawezi kuikimbia historia yake na Diamond. Ni kitu kipo na walikuwa marafiki na familia ."

Muhtasari

• "Harmonize na Diamond bado ni marafiki, sema tu kilichoisha labda ya ushirikiano wa pamoja katika biashara ya muziki, lakini mambo mengine ni yale yale."

mamake Diamond na Harmonize bado ni marafiki wakubwa.
mamake Diamond na Harmonize bado ni marafiki wakubwa.
Image: Instagram

Baada ya wiki moja ya uvumi kuwa Harmonize anatoka kimapenzi na dadake Diamond, Esma Platnumz, sasa mapya yameibuka kwamba msanii huyo pia ana uhusiano mzuri tu na Mama Dangote, ambaye ni mamake na Esma na Diamond.

Rafiki wa karibu wa Harmonize, DJ Seven alifichua haya wakati wa mahojiano ya kipekee na Sky ambapo alisema kwamba Harmonize mara kwa mara huongea na Mama Dangote kwa njia ya simu.

Kulingana na Seven, hakuna uadui uliopo baina ya Konde Gang na Wasafi kama ambavyo wengi wanachukulia kwani kilichotokea ni Harmonize na Diamond waliacha kufanya biashara ya muziki pamoja lakini katika mambo mengine hakuna kilichoharibika.

“Ukweli ni kwamba Harmonize na Diamond ni marafiki, sema tu ni biashara ya muziki waliacha kufanya pamoja. Harmonize hawezi kuikimbia historia yake na Diamond. Ni kitu kipo na walikuwa marafiki na familia. Mimi nishangai kwa sababu nimewaona mara kibao. Itakuja tu kutokea Diamond na Konde Boy wakutane tu na kula chakula pamoja,” DJ Seven alifunguka.

Alisema kuwa katika maisha hakuna chuki baina ya familia mbili ambazo ziliwahi kuwa pamoja na hivyo mama Dangote hana chuki na Harmonize hata kidogo.

“Kuna siku moja nimeona Harmonize amempigia simu Esma na alikuwa na Mama Dangote na akamwambia bwana niko na mama hapa, Harmonize akamwambia hebu nipe nimsalimie na waliongea. Hicho ni kitu ambacho nimeona kwa macho yangu,” Seven alisema.

Sekeseke hizo zilianza pale ambapo Harmonize alidhibitisha kwamba sauti ya kike ambayo inasikika kwenye wimbo wake na DJ Seven wa Say Yes ni ya Esma.