Amber Ray aibuka na picha nzuri za ujauzito katika hatua za mwisho kuelekea kujifungua

"Nguvu ya kweli ni kujipenda na kujiamini huku bado udhaifu wako ukionyeshwa hadharani," Ray alisema.

Muhtasari

• Mwanasosholaiti maarufu Amber Ray, alishirikisha picha yake ya ujauzito uliokomaa kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Instagram
Image: Amber Ray

Mwanasosholaiti maarufu Amber Ray, alishiriki picha yake ya ujauzito uliokomaa kwenye ukurasa wake wa Instagram katika muonekano wa kutamanisha.

Ray katika hiyo picha aliyopakia kwenye ukurasa wake wa Instagram alikuwa amevaa nguo ya manjano na kofia ya njano huku akionyesha ujauzito wake uliokomaa.

Katika picha hiyo mpya, mamake Gavin alidokeza kuwa ingawa udhaifu wake unaonyeshwa hadharani basi nguvu ya kweli ni kujipenda na kujiamini.

"Nguvu ya kweli ni kujipenda na kujiamini huku bado udhaifu wako ukionyeshwa hadharani," Ray alidokeza.

Mashabiki wake Ray kwenye mtandao wa Instagram, walimwonyesha mapenzi kwa muonekano ule huku wengine wakimtania na wengine wakimrushia vijembe.

"#WANGU ❤️," aliandika mchumba wake Amber, Kennedy Rapudo na kumalizia na emoji za mapenzi.

"Mrembo sana, tunafurahi kwamba ulituchagua ili tukuandalie kumbukumbu nzuri ❤," Fiestahousematernity aliandika.

"Ulisema kabisa hautafura mapua😂😂❤️," aliandika Tashleytugi.

"Zaa sasa tumechoka kuona hi mimba jamani," Mwaura8455 aliandika.

"Kumbe uko sura mbaya hivi😂😂😂😂," mwingine aliuliza.

Mchumba wake Kennedy Rapudo aliongezea katika picha hiyo na kuelezea kuwa hana stretch marks kwa hisani ya bidhaa zinazopatikana  katika Ray Irish Moss.