Katibu mwandamizi Charles Njagua adai kuwa tajiri kuliko Akothee na Harmonize

Jaguar alikua ameacha kuimba kwa muda sasa ambapo alikua akihudumu kama mbunge wa Starehe.

Muhtasari

• Jaguar akizungumza na wanahabari kuhusu kibao chake kipya akimshirikisha  msanii wa Tanzania Lava Lava alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa utajiri wake.

• Jaguar aliongeza amekuwa katika tasnia ya muziki nchini kwa muda wa zaidi ya miaka 15.

Katibu mwandamizi wa Wizara ya Vijana, Sanaa na Michezo Charles Njagua amesema kuwa ataastaafu kama akothee na Harmonize wana utajiri kumshinda.

Charles Njagua maarufu Jaguar, akizungumza na wanahabari kuhusu kibao chake kipya alichomshirikisha msanii wa Tanzania Lava Lava alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa utajiri wake.

“Kuna orodha iliyochapishwa hivi majuzi na ulikuwa nambari ya pili Kenya kama msanii Tajiri zaidi Kenya namba 7 katika wasanii wa Africa Mshariki na ripoti ile ilisema una thamani ya takriban shilingi millioni 958.3, je hiyo ni ukweli?” aliuliza mwanahabari mmoja.

Jaguar alijibu “ unaona Harmonize ako namba sijui ngapi na Akothee ako namba moja, lakini mimi naeza apa kama Harmonize na Akothee wamenishinda kwa utajiri nitaacha mziki leo”

Jaguar aliongeza kuwa amekuwa katika tasnia ya muziki nchini kwa muda wa zaidi ya miaka 15.

Aliwakashifu Akothee na Harmonize kwa kununua magari na mali ili kuonyesha utajiri wao na kusema kuwa yeye amewekeza kwa muda sasa.