Kiingereza cha Diamond chageuka gumzo kubwa mitandaoni

Kingereza cha Diamond kwenye Young Famous na African kilizua maoni tofauti tofauti miongoni mwa mashabiki wake.

Muhtasari

• Baadhi ya mashabiki walionekana wakimtania alivyozungumza Kiingereza huku wengine walionekana wakimpongeza katika kujaribu kuzungumza Kiingereza chenyewe.

Maoni ya mashabiki kuhusu kiingereza cha Diamond katika sehemu ya pili ya young famous na African
Diamond Maoni ya mashabiki kuhusu kiingereza cha Diamond katika sehemu ya pili ya young famous na African
Image: instagram

Kiingereza cha mwanamuziki Naseeb Abdul Juma almaarufu Diamond Platinumz katika sehemu ya pili ya filamu ya Young Famous na African kilizua maoni tofauti tofauti miongoni mwa mashabiki wake.

Chini ya kipande cha video ya filamu hiyo kilichochapishwa kwenye Instagram, baaadhi ya mashabiki walionekana wakimtania alivyozungumza Kiingereza huku wengine walionekana wakimpongeza katika kujaribu kuzungumza Kiingereza chenyewe.

Tazama baadhi ya maoni;

"To jump into my family kwani huyo ni chura hadi aruke?? Poor in English," aliandika Emanueldunia akimalizia na emoji za kicheko.

"Lugha ni ile ile tofauti matamshi yaani Kiingereza cha mzungu tofauti na wanachoongea nchi zingine, skiza Wanaijeria wanavyoongea au hata wahindi kwaiyo sio ajui Kiingereza shida ni matamshi yake yaani kama anaongea Kiswahili," Salumviatu aliandika.

"Kwenye hii series wamuache tu mondi aongee Kiswahili anateseka sana jamani hata anayemsikiliza hamulewi ila tu anajikaza," Pinah_65 aliandika huku akimalizia na emoji za kicheko.

"Tatizo Simba analazimisha aongee Kimarekani lakini yupo vizuri,,,,unyama sana," ajboy_boy aliandika.

"Iko ndicho Kiingereza chetu bongo we ongea simba kikubwa wameelewa basi inatosha," 7857_sebastian aliandika kwa mbwembwe.

"Ilikua ni lazima uongee kizungu Shee Mansur," Vee_bee aliuliza.

"Diamond amejaribu katika kuzungumza Kiingereza," Roseamor aliandika.

"Jamani....si uongee tu Kiswahili uweke na mkalimani ili mambo yasiwe mengi?..." Jaynezshaban aliandika.

Katika moja ya matukio kwenye filamu hiyo ya Young Famous na African, staa wa bongo Diamond Platnumz alionekana akibusiana kimahaba na mwanamuziki wa Ghana Francine Koffie almaarufu Fantana.

“Nilijiona mimi ndiye bora kwa kubusu, hadi nilipombusu Fantana,” Diamond alisema kuhusu tukio hilo la kubusiana.

Alibainisha kuwa busu la Fantana lilikuwa zaidi ya busu.

"Hakuwa ananibusu, alikuwa akinila!" alisema.

Diamond aliweka wazi kuwa busu la malkia huyo wa Ghana lilikuwa bora zaidi kuwahi kupokea katika miaka yote 32 ya kuwepo kwake.