ULIMWENGU WA MUZIKI

Rayvanny awatania mabinti wasio na viuno

Kama una kiuno,nengua umpe ushindani Baby Drama

Muhtasari

•Kama ni mdada na una kiuno basi usipofanya hii ‘challenge’ #gwedegwede #gwedegwedechallege, hatutendei haki kwa kweli.

•Katika video inayosambaa ya Gwedegwede kwenye Tik Tok, Rayvanny ameonekana kupendezwa na jinsi @baby drama69 anavyonengua kiuno chake.

Rayvanny na mkewe Fahyma
Image: INSTAGRAM// RAYVANNY

Mwanamuziki Raymond Shaban Mwakakyusa maarufu Rayvanny kwa mara nyingine amesikika akiwatania mabinti wasio na viuno katika mitandao ya kijamii.

Katika video inayosambaa ya Gwedegwede kwenye Tik Tok, Rayvanny ameonekana kupendezwa na jinsi @baby drama69 anavyonengua kiuno chake na kisha akadakia iwapo wapo mabinti wenye viuno basi wajitokeze washindane naye.

“Kama ni mdada na una kiuno basi usipofanya hii ‘challenge’ #gwedegwede #gwedegwedechallege, hatutendei haki kwa kweli.” Rayvanny alikiri.“ Oyaa hili goma mwanangu @badest47 lina nini??Mbona noma sanaa? @baby drama 69 hii nayo uliua. Alidakia ‘Chui’ kama anavyojiita Rayvanny siku hizi.

Ingawa nyota huyo wa Tanzania alianza usanii  wake tangu akiwa katika shule ya upili, aliingia kwenye ulingo wa muziki kihalisi mwaka wa 2016 baada ya ngoma yake ya “Kwetu” iliyomfanya kujulikana eneo la Afrika Mashariki.

Video ya mwana muziki huyu akimshirikisha Zuchu ‘ I miss you’ iliyovuma sana mwaka 2022 ilifanikisha staa huyo kupata wafuasi wengi zaidi ikilinganishwa na miaka ya hapo awali.