Jackie Matubia awasikitikia wanawake ambao wanawaamini wanaume

"Eti aliniambia yeye na Ex wake ni marafiki tu, wewe bado unaamini wanaume hadi leo hii 2023?" Jackie Matubia alishangaa.

Muhtasari

• Matubia aliashiria kwamba wanaume wengi ni waongo katika kile ambacho wanawaambia wapenzi wao.

• Pia alionekana kuwashauri wanawake kutoamini katika kila kitu ambacho wanaume huwaambia, haswa likija ni suala la urafiki na wanawake wengine.

Jackie Matubia awasikitikia wanawake wanaowaamini wanaume.
Jackie Matubia awasikitikia wanawake wanaowaamini wanaume.
Image: Instagram

Mwigizaji Jackie Matubia amezidi kutoa vidokezo vya kila aina kwamba huenda mapenzi yao na baba wa mtoto wake wa pili, Blessing Lung’aho yalivunjika.

Matubia katika siku za hivi karibuni baada ya kukabwa koo na mashabiki ambao walitaka kujua alipo Lung’aho, amekuwa akipakia mwendelezo wa video za kuwashambulia wanaume na kuwadunisha.

Mwigizaji huyo katika klipu ambayo ameipakia kwenye YouTube yake mapema asubuhi ya Jumatano, alionekana kuashiria kabisa kwamba mwanamke ambaye anawaamini wanaume mpaka leo hii ya mwaka 2023 huenda pengine hajielewi ama amefanyiwa ulozi na uzamwamwa.

Katika klipu hiyo, Matubia alikuwa anaigiza sauti ya mwanammke mmoja ambaye alikuwa anamjibu mwenzake ambaye alisema kuwa mume wake alimwambia yeye na aliyekuwa mpenzi wake bado ni marafiki tu na wala hakuna kingine kinachoendelea kati yao.

Kwa kujibu, sauti hiyo ya mwanamke wa pili ilimsikitikia huyo kwa kumuuliza kwa kebehi kwamba ni kwa nini anawaamini wanaume mpaka karne hii na usasa huu wa 2023.

“Unaamini wanaume? Mpaka usasa huu wote wa 2023?” Sauti hiyo ambayo Matubia alikuwa anaiga ilisikika ikisema kwa sikitiko.

Matubia alidokeza hili siku chache tu baada ya kufichua sura ya binti yake kwa mara ya kwanza, Zaidi ya miaka miwili tangu kubarikiwa na mtoto huyo pamoja na mpenzi wake Lung’aho.

Wikendi iliyopita, Matubia pia alionekana akijivinjari kwenye safari maalum ya ndege na watoto wake wawili, ikiwa ni sehemu ya mipangilio na maandalizi ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya binti yake, na kawa ambavyo imekuwa kawaida katika wiki za hivi karibuni, Lung’aho hakuwepo naye kuona binti yao akipiga hatua ya muhimu maishani.

Matubia amekuwa akikwepa kujibu swali la nini kilitokea au nini kinaendelea kati yake na Lung’aho kiasi kwamba hawaonekani pamoja na wala hataki kumzungumzia, ila kwa asilimia kubwa ametoa vidokezo kuwa huenda kuna ufa katika mapenzi yao.

Jackie Matubia awasikitikia wanawake wanaowaamini wanaume.
Jackie Matubia awasikitikia wanawake wanaowaamini wanaume.
Image: Instagram
Jackie Matubia awasikitikia wanawake wanaowaamini wanaume.
Jackie Matubia awasikitikia wanawake wanaowaamini wanaume.
Image: Instagram
Jackie Matubia awasikitikia wanawake wanaowaamini wanaume.
Jackie Matubia awasikitikia wanawake wanaowaamini wanaume.
Image: Instagram