Je, wafahamu kwa nini Alikiba hapendi kutembea na 'bodygurads'? jamaa yuko vizuri!

Kwa wasanii wote wakubwa wa Bongo, Alikiba ndiye msanii wa pekee ambaye ni nadra sana kumuona amezungukwa na walinzi wenye misuli iliyotuna.

Muhtasari

• Wengi wa wasanii hao wakubwa akiwemo Diamond Platnumz, Harmonize, Rayvanny, Nandy, Mbosso, Zuchu na wengine huwa wanaonekana wamezingira pakubwa na walinzi.

Alikiba aonekana na bastola, jinsi anavyojilinda
Alikiba aonekana na bastola, jinsi anavyojilinda
Image: Instagram

Kwa muda mrefu, wasanii wa ukanda wa Afrika Mashariki haswa wale wa kutoka bongo wamekuwa wakichagiza mambo haswa wanapokuwa katika shughuli za nje hadharani kwenye umati.

Wengi wa wasanii hao wakubwa akiwemo Diamond Platnumz, Harmonize, Rayvanny, Nandy, Mbosso, Zuchu na wengine huwa wanaonekana wamezingira pakubwa na walinzi wenye mapande sita, misuli iliyotuna, macho ya kutisha na mavazi ya ulinzi kabisa.

Walinzi hao aghalabu huwazuia watu dhidi ya kuwakaribia wasanii hawa, lakini kuna msanii mmoja ambaye ni nadra sana kumuona akiwa na ulinzi mkali wa aina hii – Alikiba.

Wengi wamekuwa wakijiuliza ni kwa nini labda Alikiba hapendi kuwa na walinzi licha ya kuwa ni mmoja kati ya wasanii wakubwa sana kuwahi kutokea na ambao wanafanya vizuri ajabu Zaidi ya miongo miwili kwenye gemu.

Ifahamike kwamba Alikiba ni msanii mhafidhina sana kiasi kwamba si rahisi mtu kuweza kujua mambo yake ya kibinafsi yeye huyaendesha aje, kwa hiyo imekuwa vigumu hata kwa wanahabari kumuuliza swali hilo kuhusu ulinzi wake.

Lakini swali hilo angalau limepata ufumbuzi japo kwa kiduchu, na si kwa msanii huyo kulizungumzia bali ni katika kitendo cha picha ambapo alionekana akiwa ba bunduki yake aina ya bastola akiwa ameiweka vizuri kwenye kiuno chake.

Alikiba alikuwa anashiriki hafla ya kupiga picha na mrembo Niffer katika harakati ya kupigia upato jezi za ‘Team Kiba’ ambazo ziko madukani kuuzwa kama njia moja ya kuchangia katika wakfu wa kuwasaidia watoto njiti.

Katika video hiyo ambayo Niffer alipakia kwenye Instagram yake, walionekana wakitaniana utadhani ni wapenzi na ukimuangalia vizuri Alikiba kama umebahatika kuona video hiyo, kiunoni upande wa nyuma kunaonekana kuna kitu ambacho kimefura nje hivi, japo kimefunikwa na jezi yake.

Lakini walipozunguka na kuonekana kama wanaondoka hivi, kamera iliwanasa upande wa nyuma na wakati huu jezi ya Alikiba ilikuwa imeinuka juu kidogo na kuweka wazi kitu kile ambacho kilikuwa kinaonekana kufura.

Kwa ukaribu inaweza onekana bastola ambayo Alikiba alikuwa ameiweka vizuri kwenda ndani ya suruali yake ndefu, na wengi walistaajabu na wakati huo huo kupata majibu kuhusu jinsi msanii huyo anavyojilinda licha ya wengi kudhani kwamba hana ulinzi wowote kwa kumuona wa kawaida bila walinzi.