Mkewe Christiano Ronaldo kupata shilingi milioni 15 kila mwezi ikiwa watatengana - Ripoti

Malipo ya kila mwezi ya Rodriguez yanasemekana kutegemea yeye kuwa mama wa watoto wote watano wa Ronaldo - sio tu binti wale wake wa kibaolojia.

Muhtasari

• Wanandoa hao waliondolewa katika sheria za Saudia zinazozuia wenzi ambao hawajaoana kuishi pamoja katika Ufalme huo.

Ronado kumlipa mkewe kitika kikubwa kila mwezi endapo wawili hao watavunja ndoa yao.
Ronado kumlipa mkewe kitika kikubwa kila mwezi endapo wawili hao watavunja ndoa yao.
Image: Twitter, Instagram

Georgina Rodriguez anaaminika kuwa na makubaliano ya 'kabla ya kufunga ndoa' na mpenzi wake Cristiano Ronaldo iwapo wawili hao watatengana, kulingana na ripoti nchini Uhispania.

Mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 29 amekuwa na nyota huyo wa Al-Nassr tangu Juni 2016, na wana watoto wawili pamoja, Alana Martina na Bella Esmeralda.

Rodriguez pia ni mama wa watoto wake wengine watatu: Cristiano Ronaldo Jnr, na mapacha Eva na Mateo, ambao walizaliwa kupitia mtu mwingine.

Wanandoa hao waliondolewa katika sheria za Saudia zinazozuia wenzi ambao hawajaoana kuishi pamoja katika Ufalme huo wakati Ronaldo alipofanya uhamisho wa pauni milioni 175 kwenda Saudi Pro League Januari mwaka huu.

Lakini licha ya kutofunga ndoa kihalali, kulingana na TV Guia, mipango imewekwa kati ya wanandoa hao iwapo watatengana ili kuhakikisha Rodriguez anapata usaidizi wa kifedha.

Makubaliano hayo yanaripotiwa kumiliki nyumba ya familia huko Madrid - La Finca - kwa nyota wa Yo Soy Georgina, na Rodriguez pia atapokea malipo ya kila mwezi ya £85,900 (€100,000) sawa na shili ngi milioni 15 kila mwezi kwa maisha yake yote.

Ronaldo alitajwa kuwa mwanariadha anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani na Forbes mwanzoni mwa Mei, huku mapato yake ya mwaka huu yakitajwa kuwa juu ya £109m.

Hii ni mara ya tatu kwa mshambulizi huyo wa zamani wa Manchester United kuingia katika orodha ya matajiri wa kila mwaka ya jarida hilo, na kiasi chake cha kushangaza kinasemekana kuwa idadi kubwa zaidi ya mwanasoka katika historia.

Malipo ya kila mwezi ya Rodriguez yanasemekana kutegemea yeye kuwa mama wa watoto wote watano wa Ronaldo - sio tu binti wale wake wa kibaolojia - mbele ya sheria.