Conjestina aanza kazi kama mlinzi wa Sonko

Sonko amemwajiri bondia huyo anayesumbuka kama mlinzi wa usalama wake.

Muhtasari

• Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Sonko alishiriki picha ya kwanza ya Conje akiwa amevalia suti yake nyeupe ya vipande viwili, ambapo alionekana kuanza siku yake rasmi kama mfanyakazi.

• Sonko alishiriki pia video ya jinsi alivyoandamana na Conje kutoka nyumbani kwake hadi kwenye gari lake ambapo Conje alifanya kazi nzuri ya kufungua mlango wa mbele wa gari lake la kifahari.

Conjestina aanza kazi kama mlinzi wa Sonko.
Conjestina aanza kazi kama mlinzi wa Sonko.
Image: Instagram

Bingwa wa ndondi conjestina Achieng amepewa mkataba mpya wa maisha shukrani kwake  Mike Sonko.

Sonko amemwajiri bondia huyo anayesumbuka kama mlinzi wa usalama wake.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Sonko alishiriki picha ya kwanza ya Conje akiwa amevalia suti yake nyeupe ya vipande viwili, ambapo alionekana kuanza siku yake rasmi kama mfanyakazi.

"Nawacho ni Conjestina okdog Siaya kwa sababu tunabadilisha maisha. Hatuchezi siasa au PR na maisha ya Mkenya yeyote," alisema mwanasiasa huyo huku akimsifu Conje sifa kemkem.

Sonko alishiriki pia video ya jinsi alivyoandamana na Conje kutoka nyumbani kwake hadi kwenye gari lake ambapo Conje alifanya kazi nzuri ya kufungua mlango wa mbele wa gari lake la kifahari.

"Tunaenda sasa, twendeni" Sonko anaelekeza timu yake iliyosimama kando.

Wanamitandao wengi walionekana kufurahishwa sana na kitendo hicho cha Sonko hivyo, wengi wao walionekana wakimpongeza katika sehemu ya maoni.

"Tabasamu lenyewe ni Baraka, utakaa sana hii dunia Mheshimiwa 👏," aliandika Ericgotkeyss_.

"Mungu awe nawe 🙏❤️," Akotheekenya alimbariki.

"Unafanya kazi nzuri mheshimiwa hiyo ndio roho tunayohitaji kutoka kwa viongozi wengine pia mungu akubariki uendelee kusaidia wengine una roho njema 🙏," Eng.simiyu alimsifu.

"Umebadilisha sana maisha ya conje," Osakavivienne alisema.

"Hiyo ni nzuri Mheshimiwa Gavana. Nakumbuka ulikuja Maringo Estate muda fulani nyuma tulikuwa tumekosa cha kula, bahati nzuri ulipita ukatupea 1k tugawane na jirani. Hio 500 kwa kweli ilituokoa sana.Mungu aendelee kukuinua.🙏 Wewe ni baraka kwa wengi," Mbuju aliandika kwa mbwembwe.

Baada ya miezi 11 ya kuokolewa na mike Sonko, hatimaye Conjestina ameonyesha ishara za kupata nafuu na kurejea kwa ndondi.