Mambo Imechemuka! Amina Khalef adai talaka kutoka kwa Alikiba katika chapisho lake

Kukasirika kwa Amina inaonekana kusababishwa na video ya kupendeza ya King Kiba na mfanyabiashara Niffer.

Muhtasari

• Mnamo Februari 2022, Amina Khalef aliwasilisha maombi ya talaka kutoka kwa mumewe akimshtumu kwa kutokuwa mwaminifu na kuongeza kwamba alidaiwa kukabiliwa na matusi kutoka kwa wakwe zake.

• Khalef alisema juhudi za kujaribu kusuluhisha maswala ya ndoa yao ziliambulia patupu kwani mumewe alikuwa asiyeitikia, na kuhitimisha kuwa ndoa ilivunjika bila kurekebishwa.

Amina Khalef adai talaka kutoka kwa Alikiba katika chapisho lake.
Alikiba na aliyekuwa mke wake, Amina Khalef Amina Khalef adai talaka kutoka kwa Alikiba katika chapisho lake.
Image: HISANI

Mke wa staa wa Bongo Alikiba ,  Amina Khalef anadai talaka kutoka kwa mwimbaji huyo baada ya miezi kadhaa ya kuishi tofauti kama wanandoa.

Katika Instastory yake, siku ya Alhamisi, Amina aliandika akisema kuwa amechoka kutoheshimiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kings Music na ni wakati wa kusaini karatasi za Talaka na kumwacha huru.

Katika ujumbe wake, Amina alibainisha kuwa hawakuwa pamoja kama wanandoa lakini King Kiba anaendelea kukatisha tamaa.

Aliendelea kusema kuwa Kiba amekuwa akimshika mateka kwa tag ya ‘Mke wa mtu’ lakini upande wake anaendelea na maisha yake bila vikwazo.

“Nimeona kuna haja ya kuongea,nadhani hii inaenda kuwa kupita kiasi!!! Nimechoka kudharauliwa hadharani huku hawaelewi hali iliyopo’ watu wakiwa katika kivuli cha MKE WA MTU!!!

“Nimeondoka kwenye maisha yako maumivu, unyanyasaji na mengi, lakini mpaka leo HUTAKI kunipatia Talaka huku wewe ukiwa huru kufanya mambo yako na mimi ukinifunga katika kivuli cha MKE WA MTU, (Kwa jina la kulinda brandi yako ulivyosema), Kindly nakuomba SAINI. KARATASI ili nipate Talaka yangu kila mmoja aendelee kwa uhuru, Asante!,” Amina aliyechanganyikiwa aliandika.

Amina Khalef
Image: Instagram

Kukasirika kwa Amina inaonekana kusababishwa na video ya kupendeza ya King Kiba na mfanyabiashara Niffer.

Niffer amekuwa akitangaza Charity Tournament ya Kiba huku wawili hao wakiibua sintofahamu baada ya Alikiba kumfollow kwenye Instagram.

Mnamo Februari 2022, Amina Khalef aliwasilisha maombi ya talaka kutoka kwa mumewe akimshtumu kwa kutokuwa mwaminifu na kuongeza kwamba alidaiwa kukabiliwa na matusi kutoka kwa wakwe zake, ambayo anasema ilianza takriban miezi sita katika ndoa yao.

Khalef alisema juhudi za kujaribu kusuluhisha maswala ya ndoa yao ziliambulia patupu kwani mumewe alikuwa asiyeitikia, na kuhitimisha kuwa ndoa ilivunjika bila kurekebishwa.

"Ndoa imevunjika kwa kiasi kikubwa na hakuna nafasi ya kuokolewa," alisema katika karatasi zilizowasilishwa mahakamani.

Khalef alidai malipo ya kila mwezi ya Shilingi 200,000 kwa ajili yake na watoto wao pamoja na bima ya matibabu kwa wawili hao.

Amina ambaye alifunga ndoa na Kiba Aprili 2018, alimshutumu kwa kutokuwa mwaminifu na kuongeza kwamba alidaiwa kukabiliwa na matusi kutoka kwa wakwe zake, ambayo anasema ilianza takriban miezi sita kwenye ndoa yao.