Khadija Kopa asimulia safari ya muziki ya bintiye Zuchu

Khadija Kopa alisimulia kwamba Zuchu alitakiwa kujiuga na chuo kikuu kimoja China ila alisema anapenda muziki.

Muhtasari

•Zuchu kwa sasa ni mmoja wa wasanii maarufu wa nyimbo za Bongo ambaye amevutia wafuasi wake kwa nyimbo na dezi za aina yake.

Khadija azungumzia suala la bintiye Zuhura kuolewa
Khadija azungumzia suala la bintiye Zuhura kuolewa
Image: HISANI

Khadija Omari Kopa mwimbaji wa muziki wa Taarab na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Tanzania ambaye pia ni mamake mzazi msanii maarufu wa Bongo Zuchu amezungumzia jinsi ambavyo bintiye aliaanza safari yake kuwa mwimbaji.

"Binti yangu Zuchu alipenda muziki kutoka utotoni mwake ila hakupenda kutangamana na watu kilochomfurahisha sana ni kusikiza muziki kwenye runinga na kwenda studio kurekodi baadhi ya nyimbo alizoiga kutoka kwa wasanii wengine",alisema.

Mwimbaji huyu alisimulia kwamba bintiye zuchu alianza muziki wake rasmi baada ya kumaliza kusoma Diploma yake nchini India, Khadija Kopa alisimulia kwamba Zuchu alitakiwa kujiuga na chuo kikuu kimoja China ila alisema anapenda muziki na alikuwa tayari kuanza ulingo wa kuwa mtunzi .

Kwenye mazugumuzo ya moja kwa moja Khadija Kopa alidokeza kwamba baada ya Zuchu kumweleza yuko tayari alifanikisha nyota yake kwa kumpa mawaidha na kumsaidia kifedha kurekodi nyimbo zake.

Zuchu kwa sasa ni mmoja wa wasanii maarufu wa nyimbo za Bongo ambaye amevutia wafuasi wake kwa nyimbo na dezi za kipekee.