Davido adaiwa kumpeleka polisi mpiga picha ambaye amekuwa akimchafua mitandaoni

Mpiga picha huyo wa spoti amekuwa akiendeleza ngonjera mitandaoni kwamba anamdai Davido zaidi ya milioni 218 za Kinaijeria.

Muhtasari

• Katika ripoti yake, alidai kuwa alimlipa mwimbaji huyo kwa mradi na Davido alikataa kwa kutojitokeza, hivyo kumfanya kupoteza mamilioni.

Davido
Davido
Image: X

Katika wiki za hivi karibuni, mtu mmoja anayejiita mpiga picha nchini Nigeria kwa jina Abu Salami amekuwa akiendeleza mfululizo wa mashambulizi dhidi ya msanii Davido kwa kile anadai kwamba msanii huyo ana deni lake kubwa ambalo amekataa kumlipa.

Licha ya mwendelezo wa mashambulizi hayo yakiwemo kumuita maskini, Davido hajakuwa akijibu hata kidogo lakini sasa vyanzo vya habari kutoka taifa hilo vinadai kwamba huenda msanii Davido ameenda kisheria Zaidi kwa kumpeleka polisi Salami.

Kulingana na blogu hizo, Salami ameshtakiwa na Davido kwa kosa la kumfuatilia nyendo zake mitandaoni, kughushi sahihi zake na uhalifu mwingine ikiwemo kumchafulia jina kwa madai yasiyo ya kweli.

Kumbuka kwamba wiki zilizopita, mfanyabiashara huyo alijitokeza na kumwita Davido, akidai kwamba mwimbaji huyo anadaiwa naira milioni 218 na academia yake [Salami] ya soka.

Katika ripoti yake, alidai kuwa alimlipa mwimbaji huyo kwa mradi na Davido alikataa kwa kutojitokeza, hivyo kumfanya kupoteza mamilioni.

Pia aliapa kumpeleka Davido mahakamani kwa ajili ya suala hilo.

Picha ambazo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zimemuonyesha mpiga picha huyo akiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Inasemekana kwamba Salami alikiri kwenye jukwaa la X, ambalo zamani lilijulikana kama Twitter kwamba alighushi saini ya Davido na alionyesha kiburi kwa matendo yake.

Mpiga picha huyo alionekana akiandika maelezo yake alipowasili katika kituo cha polisi katika moja ya picha zilizosambaa mtandaoni.

Katika picha nyingine, Abu Salami, akiwa amevalia kaftan nyeupe, alionekana nyuma ya kaunta, akiongeza fumbo.