Hatimaye Davido aonesha picha ya wanawe mapacha akisherehekea miaka 31

Hii ni mara ya kwanza kwa Davido kuonesha picha akiwa amepakata fungu lake la thamani mikononi huku tabasamu pana likiwa limemuangaza uso mzima.

Muhtasari

• Msanii huyo hakutaja siku yake ya kuzaliwa hata kidogo siku nzima lakini alichapisha mtandao wa kijamii usiku wa manane kusherehekea.

Davido na mapacha wake.
Davido na mapacha wake.
Image: Instagram

Mwimbaji wa Nigeria David Adeleke, anayejulikana zaidi kama Davido, alitimiza umri wa miaka 31 mnamo Novemba 21 na alisherehekea kwa kushiriki picha tamu za mke wake na mapacha wachanga.

Hii ni mara ya kwanza kwa Zaidi ya mwezi mmoja baada ya yeye na mkewe Chioma kuthibitisha uvumi kwamba walijaaliwa watoto mapacha, mwaka mmoja baada ya kifo cha mwanao Ifeanyi.

Mbali na kushiriki picha za kupendeza za mapacha wake na mkewe, Chioma, pia alichapisha picha ya baba yake, Deji Adeleke.

Msanii huyo hakutaja siku yake ya kuzaliwa hata kidogo siku nzima lakini alichapisha mtandao wa kijamii usiku wa manane kusherehekea.

Kwa heshima ya hafla hiyo, mashabiki wake na washirika wa biashara walijitokeza kwenye majukwaa anuwai ya mitandao ya kijamii kuonyesha shukrani zao.

Kisha akaendelea kuonyesha uthamini wake kwa Mungu kwa ajili ya mwaka mpya ambao amepewa.

Hii ni mara ya kwanza kwa Davido kuonesha picha akiwa amepakata fungu lake la thamani mikononi huku tabasamu pana likiwa limemuangaza uso mzima.

Itakumbukwa mwishoni mwa mwaka jana, Davido alikuwa na mwisho mbaya baada ya mwanawe wa kipekee kufa maji nyumbani kwao akiwa anapiga mbizi.

Msanii huyo hakuwaji kujitokeza mitandaoni kwa Zaidi ya miezi miwili lakini alikuja kuvunja ukimya mwezi Janauri kwa kutoa albamu yake ya Timeless ambayo imepata mapokezi makubwa.