Carol Katrue achora tattoo ya Miracle Baby kifuani kuwamezesha wivu babymamas wake

Alikiri kwamba anajua Miracle Baby ana babymamas wengi ambao hata mwenyewe hana uhakika wa idadi kamili.

Muhtasari

• Alikiri kwamba anajua Miracle Baby ana babymamas wengi ambao hata mwenyewe hana uhakika wa idadi kamili.

Miracle Baby na Carol Katrue
Miracle Baby na Carol Katrue
Image: Facebook

Msanii wa Mugithi Carol Katrue ameamua kuchukua ugomvi na babymamas wa mpenzi wake ambaye pia ni msanii, Miracle Baby katika kiwango kingine baada ya kuchora tattoo ya msanii huyo kwenye kifia chake.

Mrembo huyo mama wa mtoto mmoja alifichua hili kwa kuthibitisha kabisa kuwepo kwa tattoo ya Miracle Baby na ya mwanawe kwenye kifua na kusema kwamba alichochewa na babymama wake wengi.

Katrue alisema kwamba alifanya hivyo ili kuwamezesha babymama wa Miracle Baby wivu na hasira ili nao kama kweli wanampenda wachore tattoo hata kwenye paji la uso.

“Moja ni ya Miracle Baby na nyingine ni Ronex, familia yangu. Kwa hiyo babymama mwenye anaona kama amejitambua, naye achore kwenye makalio ama kweney uso haoa, akuje tutoshane,” alisema.

Mrembo huyo alisema sababu ya kushinda akiburuzana na wapenzi wa zamani wa Miracle Baby ni kutokana na madharau ambayo wanamuonesha, akisimulia kisa cha juzi ambapo akiwa live kwenye TikTok mmoja wao alimkaripia kwa kutumia namba ngeni.

“Mimi ninaumwa, juzi nimeingie live TikTok na simu yenye natumia ndio ilikuwa na Sim Card yangu ndani, kidogo naona namba mgeni usiku, mara ya kwanza nikakata, mara ya pili sikuchukua na baadae kuangalia ni nani alikuwa ananitafuta, nikapata nimeandikiwa matusi, nilituma shilingi Mpesa nikaona ni mmoja wa babymama alimtuma,” alisema.

Carol Katrue na Miracle Baby wamekuwa wapenzi tangu msanii huyo aondoke katika kundi la Gengetone la Sailors Gang na wakaanza kuimba nyimbo za Mugithi.

Alikiri kwamba anajua Miracle Baby ana babymamas wengi ambao hata mwenyewe hana uhakika wa idadi kamili.