Cristiano Ronaldo asherehekea kufikisha miaka 39 akiwa amezungukwa na familia yake

"Nashukuru kutumia siku yangu ya kuzaliwa ya 39 kwa njia bora zaidi: nikiwa na familia yangu na kurudi kwenye uwanja wa mazoezi. Asanteni nyote kwa jumbe za kusisimua!"

Muhtasari

• Licha ya umri wake, Ronaldo bado anaimarika na haonyeshi dalili zozote kwamba anafikiria kumaliza maisha yake ya uchezaji.

Nyota wa Ureno na Al Nassr asherehekea siku yake ya kuzaliwa na familia yake
Cristiano Ronaldo// Nyota wa Ureno na Al Nassr asherehekea siku yake ya kuzaliwa na familia yake
Image: Facebook

Shujaa wa Al-Nassr Cristiano Ronaldo alikuwa katika hali ya "shukrani" alipokuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 39 akiwa na mpenzi wake Georgina Rodriguez na watoto wake.

Nyota huyo wa Ureno alifikisha miaka 39 Jumatatu na, baada ya kusherehekea na wachezaji wenzake siku hiyo, aliadhimisha hafla hiyo na familia yake Jumanne. 

Pamoja na keki tatu za siku ya kuzaliwa, mshambuliaji huyo alionyesha shada kubwa la maua alipokuwa akipewa.

Ronaldo alipiga picha pamoja na familia yake na kuwaandikia wafuasi wake kwenye Instagram: "Nashukuru kutumia siku yangu ya kuzaliwa ya 39 kwa njia bora zaidi: nikiwa na familia yangu na kurudi kwenye uwanja wa mazoezi. Asanteni nyote kwa jumbe za kusisimua!"

Licha ya umri wake, Ronaldo bado anaimarika na haonyeshi dalili zozote kwamba anafikiria kumaliza maisha yake ya uchezaji.

Amefunga mabao 20 katika mechi 18 za Saudi Pro League na pia matatu kwenye Ligi ya Mabingwa ya AFC, akiisaidia timu yake kufika hatua ya mtoano.

Nyota huyo wa zamani wa Manchester United na Real Madrid amekuwa nje kutokana na jeraha wiki za hivi karibuni lakini amerejea mazoezini na wachezaji wenzake wa Al-Nassr.

Atatumai kuhusika watakapomenyana na Al-Feiha katika Ligi ya Mabingwa ya AFC baadaye mwezi huu.