Ronaldo amnunulia mkewe saa ya shilingi milioni 16 kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa

Mwanamitindo huyo aliyegeuka kuwa mshawishi alisherehekea siku yake ya kuzaliwa mnamo Januari 27, akitimiza miaka 30.

Muhtasari

• Saa hiyo ilikuwa na mkanda wa waridi na ilikuwa na almasi katika kipochi hicho. Thamani ya saa inaaminika kuwa na thamani ya zaidi ya $100,000

Mwanasoka huyo alimnunulia mkewe zawadi ghali ya siku ya kuzaliwa
Christiano Ronado na mkewe// Mwanasoka huyo alimnunulia mkewe zawadi ghali ya siku ya kuzaliwa
Image: Instagram, Facebook

Mpenzi wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez kupitia Instagram story yake ameonyesha mashabiki wake zawadi ghali na adimu ambayo ainunuliwa na mumewe akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Rodriguez alionyesha saa nzuri yenye almasi juu yake ambayo jarida la Sportskeed liifichua kwamba ni ya thamani ya hadi dola laki moja sawa na milioni 16 pesa za Kenya kutoka kwa kampuni ya Jacob and Co.

“Saa hiyo ilikuwa na mkanda wa waridi na ilikuwa na almasi katika kipochi hicho. Thamani ya saa inaaminika kuwa na thamani ya zaidi ya $100,000,” Jarida hilo lilibaini.

Mwanamitindo huyo aliyegeuka kuwa mshawishi alisherehekea siku yake ya kuzaliwa mnamo Januari 27, akitimiza miaka 30.

Jacob and Co ni kampuni ya vito na saa ya mkono ambayo ilianzishwa mnamo 1986 na mbunifu Jacob Arabo. Kulingana na tovuti yao, Arabo amekuwa rafiki na Ronaldo tangu fowadi huyo alipokuwa nyota wa kutumainiwa siku za usoni.

Kampuni pia ina ushirikiano maalum na ikoni huyo wa Al-Nassr, mkusanyiko wa saa muhimu. Seti mbili - zinazojulikana kama Flight of CR7 na Heart of CR7 - zimeundwa na Jacob and Co na zinapatikana kwenye tovuti yao.