Charlene Ruto kutoa zawadi ya 100K na kushiriki lunch na mtu mmoja mwenye bahati

Shindano hilo linatoa nafasi kwa vijana kuonyesha ustadi wao katika kubuni nembo nzuri na mshindi atapokezwa kitika cha shilingi laki moja.

Muhtasari

• Shindano hilo linatoa nafasi kwa vijana kuonyesha ustadi wao katika kubuni nembo nzuri na mshindi atapokezwa kitika cha shilingi laki moja.

Binti Ruto
Binti Ruto
Image: facebook

Binti wa kwanza wa taifa, Charlene Ruto amezindua shindano la kibunifu ambapo anawataka vijana wenye ustadi katika kuunda nembo za kidijitali kujitokeza ili kushiriki katika shindano hilo.

Kupitia ukurasa wake wa X, Binti Ruto alisema kwamba shirika la Mtandao wa Vijana wa Kimataifa linatafuta nembo nzuri ambayo inahusiana na masuala ya vijana katika ubunifu.

Shindano hilo linatoa nafasi kwa vijana kuonyesha ustadi wao katika kubuni nembo nzuri na mshindi atapokezwa kitika cha shilingi laki moja pamoja pia na kushiriki chakula cha mchana kwenye meza moja na Charlene Ruto.

“Mtandao wa Vijana wa Kimataifa (TYPNI) unatafuta nembo bainifu inayojumuisha ari ya ujana na ubunifu. Shindano hili linatoa fursa kwa wabunifu wachanga kuonyesha vipaji vyao na kuchangia utambulisho mahiri wa TYPNI,” aliandika kwenye bango hilo kwenye mtandao wa X.