Bahati na Diana Marua washangaza mashabiki kwa kutumia mswaki mmoja kwa zamu (video)

Hatua hii ya kubadilishana mswaki kutoka kwa mdomo wa Bahati kwenda kwa mdomo wa Diana na kurudia ilivutia maoni tofauti kutoka kwa mashabiki wao.

Muhtasari

• Bahati walisema ni ishara ya mapenzi wengine wakipinga kwa kauli kwamba huo ni ukichaa katika mapenzi.

 

Bahati na mkewe Diana
Bahati na mkewe Diana
Image: Instagram

Wakuza maudhui Diana Marua na Kevin Bahati wamewaacha mashabiki na watumizi wa mtandao wa Instagram katika hali ya mshangao baada ya kupakia video wakishiriki kupiga mswaki kwa kutumia mswaki mmoja.

Wawili hao walionekana katika hali ya furaha huku kila mmoja akiuchukua mswaki huo huo mmoja kwa zamu kutoka kwa mdomo wa mwenzake.

Baadae hata kabla ya kusukutua, Diana alionekana akitaka kumbusu Bahati kabla ya wote kucheka.

Waliandika;

“Yako ni Yangu; Yangu ni Yako ❤️ Nitang’a Ng’ana Nawe 😂😂😂😂😂😂😂.”

Hatua hii ya kubadilishana mswaki kutoka kwa mdomo wa Bahati kwenda kwa mdomo wa Diana na kurudia ilivutia maoni tofauti kutoka kwa mashabiki wao.

Bahati walisema ni ishara ya mapenzi wengine wakipinga kwa kauli kwamba huo ni ukichaa katika mapenzi.

“Uongo mbaya! Siwezi kushiriki mswaki wangu 😂😂😂 afadhali mninyonge,” Njambi Fever.

“Diana siuko na bahati ,unaishi kimalaika utaenda Heaven direct,” Eddy Musomb alisema.

“Nikifika hapa mnipige risasi ya figo.” Sebastian Obk.

“Uwiiiii nimehisi kutapikaa” Zahras Choice alisema.