Vincent Mboya afikiria kutafuta penzi kwa ‘wamama’ miaka 40+... au kuwa shoga

Haya yanajiri wiki chache baada ya Georgina Njenga kumuanika kwa kumrubuni kwa shilingi elfu 3 na kujipiga kifua mitandaoni kwamba amemnunulia mrembo huyo gari.

Muhtasari

• "Wanawake waliokomaa wanaweza kuwa wazuri kwangu! Au nakutana na shoga? " aliuliza.

Vincent Mboya
Vincent Mboya
Image: Instagram KWA HISANI

Wiki chache baada ya Georgina Njenga kumuanika mitandaoni kwa kudanganya kumnunulia gari kumbe alimtumia shilingi elfu 3, YouTuber Vincent Mboya ametangaza kukoma kuwafukuzia wanawake tena kwa ajili ya penzi.

Mboya ambaye kwa sasa anaishi nchini Canada, kupitia Instagram yake, alichapisha ujumbe mrefu na kueleza sababu kuntu kwa nini ameamua kuacha kabisa kufukuzia penzi kutoka kwa kina dada.

Kijana huyo aliweka wazi kwamba wanawake kwa mara kadhaa wamekuwa wakijaribu kumuangusha na kumrudisha nyuma lakini Mungu amekuwa akimnusuru na sasa ameamua kujitenga kabisa na mtego huo wa wanawake.

“Inatosha, acha nimwaga kila kitu nje! Mbali na wanafamilia yangu upendo wangu kwa wanawake umetoweka kabisa. Wanawake ni wabaya sana! Wanawake ni majeruhi! Wanawake wamejaribu kila kitu kuniweka chini lakini Mungu amejitokeza kwa ajili yangu!” Mboya alisema.

Mbona alionekana kurejelea tukio ambalo alikesha korokoroni kwa siku kadhaa mwaka jana na kusema kwamba ni mwanamke ambaye walikuwa wapenzi na baada ya kutengana, akamsingizia ubakaji.

“Ninakutana na mwanamke tuna kitu lakini baada ya kugombana anafikiria kuja na hadithi ya uwongo kisha kwenda hadharani atanimaliza na atapata, hata hivyo anapata umakini kwa siku basi kazi yangu bado inaendelea. Nimeona na kusikia yote kutoka kwa wanawake!” alisema.

Kijana huyo mwenye umri wa 20s alitathmini iwapo atasalia bila mwanamke hadi kufa au abadili wimbi na kuzamia katika penzi la wanawake wenye umri wa miaka 40 kwenda mbele, akisema kwamba kizazi cha sasa kimemtaabisha kushoto-kulia.

“Siri yangu sasa ni je nikae single mpaka nife? Au ninajaribu kuchumbiana na wanawake wakubwa 40years+? Kwa sababu kizazi kipya kimenifanya kupita katika mengi, wanawake waliokomaa wanaweza kuwa wazuri kwangu! Au nakutana na shoga? Labda wanawake wote ni sawa, vijana na wazee! Kwa sababu mimi ni binadamu nahitaji upendo na mapenzi!”