Georgina Njenga amwanika Vincent Mboya kwa kumtumia 3k kununua zawadi ya gari

Kwa mujibu wa Mboya, alimtumia Georgina pesa nyingi kujinunulia gari la kifahari kama zawadi ya Valentine, baadae ikagundulika alimtumia shilingi elfu 3 tu!

Muhtasari

• Kwa mshangao wa wengi, ujumbe huo ulionesha Mboya alimtumia Georgina Njenga shilingi elfu 3 pesa za Kenya na kudai kwamba ni zawadi ya kununua gari.

Georgina na Mboya.
Georgina na Mboya.
Image: Maktaba

TikToker Georgina Njenga amemwanika mwanablogu wa YouTube Vincent Mboya baada ya kijana huyo aliyeko nchini Canada kudai kwamba alimtumia pesa kununua gari la kifahari kama zawadi ya siku ya wapendanao – Valentino.

Mboya alikuwa ametamba awali akidai kwamba amemnunulia Georgina Njenga zawadi ya gari la kifahari kumsherehekea siku ya wapendanao.

Hata hivyo, Georgina Njenga alijitokeza na kukanusha vikali madai hayo ya Mboya na kusema kwamba mwanamume huyo aliyeondoka kwenda Canada mwaka jana hafai hata chembe kuwa mpenzi wake.

Baada ya zoo hio kuonekana kuwaingiza wengi kwenye chaka, mpenzi wa zamani wa Tyler Mbaya aliamua kutenganisha mbivu na mbichi kwa kuweka wazi ujumbe wa muamala wa M-Pesa ambao Mboya alidai alimtumia pesa za kununua gari.

Kwa mshangao wa wengi, ujumbe huo ulionesha Mboya alimtumia Georgina Njenga shilingi elfu 3 pesa za Kenya na kudai kwamba ni zawadi ya kununua gari.

Njenga alisema kwamba Mboya akiendelea kudanganya kuhusu kumnunulia zawadi ya gari kama kumuonyesha mapenzi basi atamwanika na kumuumbua vibaya.

“Kama hii ndio anatuma Valentines gari ndio atanunua? Mpenzi wangu anaweza kufanya vizuri kumliko Mboya, Mboya ni mzuri lakini yeye sio type yangu, atafute tu kwingine,” Njenga alisema kwenye screenshot hiyo.