Diamond awaasa vijana kutumia changamoto na kheri za maisha yake kujipa motisha kimaisha

Diamond alijinadi kuwa kijana mkomavu na mwenye ujasiri wa kipekee katika kupambania riziki za kimaisha, tangu akiwa mdogo, akiwataka vijana wenzake kufuata nyayo zake katika mkondo wa mafanikio.

Muhtasari

• Diamond alijinadi kuwa kijana mkomavu na mwenye ujasiri wa kipekee katika kupambania riziki za kimaisha,

Diamond Platnumz
Diamond Platnumz
Image: Facebook, Instagram

Mburudishaji tajika wa muziki kutoka Tanzania, Diamond Platnumz amewashauri vijana wenzake na wale wanaokua sasa kutumia changamoto na kheri za maisha yake ya kupanda na kushuku kama motisha katika maisha yao ya utafutaji wa riziki.

Msanii huyo kupitia Instagram, aliandika ujumbe mrefu alihadithia jinsi maisha yake yalivyoanza kwa taabu na kukwea ngazi pole pole mpaka sasa amejipata kwenye kilele cha maisha mazuri kutokana na bidii zake katika utafutaji riziki kupitia muziki.

Aliwataka vijana kujifunza kutokana na changamoto zake hizo lakini pia kutoka kwa mafanikio yake kama kujipa motisha kwamba sio siku zote mtu utakuwa katika maisha ya chini, kwani ukijibidiisha na pamoja na nidhamu, utafanikiwa kama yeye.

Vijana Wenzangu, Sina kikubwa cha kuwapa ila kuwasihi kutumia Changamoto na Kheri za Maisha yangu kama moja ya Motisha ya Maisha yenu kwenye mbio za kujikomboa Kimaendeleo….Muamini ya kwamba kila kitu kinawezekana Chini ya jua… ila tu Inataka Utayari, Juhudi, Uvumilivu, Ubunifu, Adabu, kutokukata tamaa na Siku zote Kuepuka Kuwa Chanzo cha Tatizo kwa kitu ama Mtu yoyote ili uwe na Haki na Ulinzi wa Mungu Duniani na Akhera,” Diamond aliandika.

Diamond alijinadi kuwa kijana mkomavu na mwenye ujasiri wa kipekee katika kupambania riziki za kimaisha, tangu akiwa mdogo, akiwataka vijana wenzake kufuata nyayo zake katika mkondo wa mafanikio.

“Vijana wenzangu, Huyo Kijana Unaemuona Hapo ni Jasiri na Mkomavu Kwelikweli na ndio moja ya Nguzo za Kuwepo hapo hadi leo, Kama yeye anaweza basi naamini sisi Wote tunaweza!…InshaAllah Mwenyez Mungu atujaalie ijumaa ya leo ikawe yenye Kheri na kutufanikisha Ndoto zetu wote,” aliongeza.