Eric Omondi amsherehekea mkewe kwa ujumbe mtamu siku yake ya kuzaliwa

Omondi alisema kwamba mrembo huyo kwa kumzalia binti mrembo Kyla, alimpa zawadi ya thamani Zaidi ambayo kwa asilimia yote ilifanya maisha yangu kuwa kamili.

Muhtasari

• Eric Omondi alimkumbusha mrembo huyo kwamba anavyosherehekea siku yake ya kuzaliwa leo, fahamu kwamba hakuna chochote atakachoshindwa kumfanyia.

 

Eric Omondi na mpenziwe Lynne.
Eric Omondi na mpenziwe Lynne.
Image: Facebook

Mchekeshaji aliyegeuka kuwa mwanaharakati wa haki za kibinadamu, Eric Omondi amemsherehekea mkewe Lynn kwa ujumbe wa kutamanisha siku yake ya kuzaliwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Eric Omondi alichapisha picha ya mrembo huyo mama wa mtoto mmoja na kumtungia ujumbe mrefu wenye makopakopa mengi akimsifia jinsi alivyo muhimu kaitka maisha yake.

Omondi alisema kwamba mrembo huyo kwa kumzalia binti mrembo Kyla, alimpa zawadi ya thamani Zaidi ambayo kwa asilimia yote ilifanya maisha yangu kuwa kamili.

Omondi alisema kwamba Lynn anastahili vitu vyote vizuri duniani na Zaidi kwa kumfanya kuitwa baba.

“Mpenzi Wangu, Malkia Wangu, Mwandani Wangu. Namshukuru Mungu Kila Siku Kwa Kukuleta Katika Maisha Yangu. Wewe ni ZAWADI BORA kabisa niliyowahi Kupokea na ukanipa ZAWADI NZURI KULIKO WOTE... Malaika Wetu Mpenzi @kyla.omondi UMENIFANYA MAISHA YANGU KUKAMILISHA. Unastahili Ulimwengu na ZAIDI,” Omondi aliandika.

Eric Omondi alimkumbusha mrembo huyo kwamba anavyosherehekea siku yake ya kuzaliwa leo, fahamu kwamba hakuna chochote atakachoshindwa kumfanyia.

“Unaposherehekea Siku yako ya Kuzaliwa LEO ujue tu kwamba hakuna kitu ambacho nisingefanya kwa ajili yako. Nakutakia MAISHA ELFU zaidi. NAKUPENDA  ️ Babyy. HAPPY BIRTHDAY BABYYYY🌹🌹❤🎂🎂😍😍😋😋👸👸. FURAHIA LIKIZO YAKO...UNASTAHILI DUNIA NZIMA,” alimaliza.

Penzi la Omondi na Lynn limekuwa likizungumziwa na watumizi wa mitandao ya kijamii kutokana na utofauti mkubwa uliopo baina yao.

Eric anamuacha Lynn kwa Zaidi ya miaka 20, jambo ambalo baadhi wamekuwa wakimkosoa lakini miezi kadhaa iliyopita katika mahojiano na Radio Jambo, aliwashauri vijana wa kiume kuhakikisha wanaoa wanawake ambao ni nusu ya umri wao ili penzi kudumu.

“Kaka usioe mwanamke ambaye yuko kwenye mabani ya umri mmoja na wewe kiumri, eti nyote mko katika miaka ya 20s, hiyo imekufa kabla ifike…” Omondi alisema.

“Wanawake huwa wanakomaa mapema na haraka, mwanamke wa miaka 24 ni wa mwanamume wa miaka 40. Mimi ninependekeza uoe mwanamke ambaye ako na nusu ya umri wako, na ikienda sana awe na robo ya umri wako…. Kama uko na miaka 30 achana na wanawake wa miaka 29 kuteremka hadi 20….” Omondi aliongeza katika mahojiano hayo na Massawe Japanni.