Libianca alazimika kusitisha shoo ya Marekani kufuatia kutishiwa maisha na wapiganaji wa Kameruni

"Jamani, nitaahirisha ziara yangu kutokana na vitisho vya kuuawa ambavyo nimekuwa nikipokea. Ninakataa kughairi nahitaji tu muda wa kuchukua tahadhari muhimu nakupenda!" alisema.

Libianca
Libianca
Image: Instagram

Libianca, msanii wa kike anayefanya vizuri kutoka Cameroon ameripotiwa kuchukua uamuzi wa kusitisha msururu wa shoo zake Amerika Kaskazini kutokana na kile alitaja kuwa ni vitisho kwa maisha yake.

Kwa mujibu wa Cameroon News Agency, mrembo huyo aliyepata umaarufu na ufanisi mkubwa kutokana na wimbo wake wa ‘People’ alisema Ijumaa kwamba timu yake iliamua kuchukua hatua hizo kutokana na makundi mawili ambayo yanaendelea kupigana katika kanda za Kaskazini Magharibi na Kusini Magharibi mwa Nigeria ambao wanamtishia maisha kwa kuonesha bendera ya Kameruni.

Libianca aliandika ujumbe huo kwa mashabiki wake wa North America ambao walikuwa wamemsubiri kwa hamu kuu, akieleza kutofurahishwa kwake kwa kutotimiza ahadi yake kwao.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, moja kati ya vitisho hivyo vilitokana na kiongozi mpiganaji mmoja ambaye yuko Ubelgiji kwa jina Sam Thomas Achoa ambaye anaendesha ukurasa wa propaganda mitandaoni.

"Jamani, nitaahirisha ziara yangu kutokana na vitisho vya kuuawa ambavyo nimekuwa nikipokea. Ninakataa kughairi nahitaji tu muda wa kuchukua tahadhari muhimu nakupenda!" alisema.

Libianca alisema kwamba vitisho hivyo vilizidi baada ya kumaliza shoo za Australia lakini pia akaonesha Imani yake kwamba Amani siku moja itarejea katika maeneo hayo mawili na Kameruni kuwa taifa moja lenye mshikamano.

Hii hapa ni barua yake kwa mashabiki wake;