Rayvanny: Wimbo wa ‘Hongera’ hauhusiani na ex wangu Paula kuwa na mimba ya Marioo

“Marioo ni damu yangu, familia na anatarajia mtoto. Paula anatarajia mtoto kwa hivyo ninawapongeza. Wimbo huo ni maalum kwa wanawake wajawazito." Rayvanny alisema.

Muhtasari

• “Wimbo huu ni maalum kwa wajawazito na pia wale ambao tayari wamejifungua. Nimeutoa wimbo huu kwa wanawake wote wajawazito na wale waliojifungua.” Aliongeza.

• Msanii huyo aidha alisema hana bifu lolote na Marioo, ambaye ni mpenzi mpya wa ex wake Paula lakini akasema kuwa hana mazungumzo na Paula kwa vile ni mke wa mtu.

Rayvanny awatolea wimbo wa pongezi Marioo na Paula
Rayvanny awatolea wimbo wa pongezi Marioo na Paula
Image: Instagram

Msanii wa Next Level Music, Rayvanny amejitokeza na kupuuzilia mbali madai kwamba wimbo wake mpya wa ‘Hongera’ unalenga kutuma ujumbe wa majungu kwa aliyekuwa mpenzi wake, Paula Kajala baada ya kuweka wazi kuwa anatarajia mtoto na mpenzi mpya, Marioo.

Akizungumza na waandishi wa habari za burudani, Rayvanny alisema kwamba wazo zima la tungo hiyo inayomhongera mwanamke mjamzito anayetarajia kuitwa mama lilitokana na picha aliyoona jinsi mwanamke mjamzito alivyokuwa akifanyiwa ndani ya ndege wakati wanasafiri pamoja.

Rayvanny pia alisema wimbo huo ni kwa kina mama wote ambao wamewahi beba ujauzito, akitaja mchakato mzima kuwa si jambo rahisi kwa mtu kustahimili ujauzito kwa miezi tisa lakini pia uchungu wa leba hadi kumtotoa mwana.

“Kuhusiana na wimbo wa ‘hongera’, nilikaa siku nilikuwa kwenye ndege. Kuna mama mjamzito akawa anapewa treat kwa sababu ni mjamzito nikakaa nikiwaza kina mama wanapitia changamoto nyingi sana mpaka wanatuzaa sisi.”

“Kuna wanapenda ujana aende klabu azunguke lakini mwanamke akiamua wacha nizae maanake anakitunza hicho kiumbe, kukaa na mzigo miezi tisa si kitu kidogo, mateso ya leba na akili sio kitu kidogo na mama zetu ndio wanazaa mashujaa, marais, masuperstar, talents tofautitofauti, mapilot kwa hio nikasema kwa nini nisifanye kitu ambacho ni cha kuwapongeza wamama,” baba huyo wa mtoto mmoja wa kiume alisema.

“Wimbo huu ni maalum kwa wajawazito na pia wale ambao tayari wamejifungua. Nimeutoa wimbo huu kwa wanawake wote wajawazito na wale waliojifungua.” Aliongeza.

Msanii huyo aidha alisema hana bifu lolote na Marioo, ambaye ni mpenzi mpya wa ex wake Paula lakini akasema kuwa hana mazungumzo na Paula kwa vile ni mke wa mtu.

“Marioo ni damu yangu, familia na anatarajia mtoto. Paula anatarajia mtoto kwa hivyo ninawapongeza. Wimbo huo ni maalum kwa wanawake wajawazito. Kwa kuwa Paula ni mjamzito, wimbo huo pia ni maalum kwake kama wengine,” alisema.