Kanze Dena amruhusu mwanawe kujiunga katika mitandao ya kijamii baada ya kuhitimu miaka 18

“Leo una kibali rasmi cha kuwa kwenye mitandao ya kijamii... Nataka ujue kuwa kumbukumbu yangu kubwa ni siku tulipomtazama Woman without Limits. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kushiriki vita yangu na kujithamini," Dena alisema.

Muhtasari

• Aidha, alimuusia kwamba amefikisha umri rasmi wa kujiunga kwenye mitandao ya kijamii ila akamuonya dhidi ya kupotea kwa maamuzi mabaya.

• Kama mama yeyote, Kanze Dena pia alimkumbusha mwanawe kutopotoka kutoka njia kuu ya Ukristo.

Kanze Dena na mwanawe
Kanze Dena na mwanawe
Image: Instagram

Aliyekuwa kaimu msemaji wa ikulu, Kanze Dena ni mama mwenye furaha baada ya mwanawe wa kiume kufikisha umri wa miaka 18.

Dena kupitia ukurasa wake wa Instagram alichapisha ujumbe mrefu na mtamu akiuambatanisha na picha za pamoja na mwanawe na kumsherehekea kwa kuwa mtoto mtiifu katika kipindi cha miaka 17 iliyopita.

Mwanahabari huyo wa zamani wa runinga ya Citizen alionyesha fahari yake kwa mwanawe kuhitimu rasmi umri wa kuwa raia wa kujifanyia maamuzi mwenyewe na kumuusia kuendeleza utiifu ambao amekuwa nao tangu utotoni.

“Bingwa wangu! umenifanya niwe na fahari. Tumepitia Majira ya baridi, Vuli, Masika na Majira ya joto na hukuwahi kubadilika. Wakati hukuwa na vitu vya kuchezea kama marafiki zako, sikuweza kukupeleka mahali pazuri kwa sababu hatukuwa nazo, na ukakumbatia wazazi wako wa kambo na ndugu zako kama bingwa ulivyo... Usitupe shida ya uzazi! ...Na Mungu alipotubariki ulibaki bila kubadilika,” Kanze alianza kumimina sifa kwa mwanawe.

Aidha, alimuusia kwamba amefikisha umri rasmi wa kujiunga kwenye mitandao ya kijamii ila akamuonya dhidi ya kupotea kwa maamuzi mabaya.

Kama mama yeyote, Kanze Dena pia alimkumbusha mwanawe kutopotoka kutoka njia kuu ya Ukristo.

“Leo una kibali rasmi cha kuwa kwenye mitandao ya kijamii... Nataka ujue kuwa kumbukumbu yangu kubwa ni siku tulipomtazama Woman without Limits. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kushiriki vita yangu na kujithamini na nilitaja kwamba nilitilia shaka kama nilikuwa mama mzuri (kama miaka 7/8 iliyopita) Ulinishika mkono, ukanikumbatia kwa kama miaka 10 "mama wewe ni bora Zaidi ambaye ningeweza kuomba kupata... wewe ni mkali lakini wewe ni rafiki yangu na najua unanipenda mummie." Maneno hayo yamerudi leo nilipokesha kuomba maombi mengine ya msimu ujao.”

“Keep on keeping on Mwana ...DONT LOOSE YOUR FOCUS ON JESUS. YEYE NDIYE NANGA YAKO KUU (utagundua hivi karibuni unapopitia maisha).”