Ommy Dimpoz amzawadi Marioo 5M kwa kumpachika mimba Paula, kumfanya Kajala kuitwa bibi

"Kutokana na hicho ulichokifanya, cha kumfanya Kajala tumuite bibi, mimi nakupa zawadi ya milioni 5,” Ommy Dimpoz alisema..

Muhtasari

• Marioo alianza kuchumbiana na Paula baada ya mrembo huyo kukatisha uhusiano wake na msanii Rayvanny.

 
• Iliarifiwa kwamba Marioo alikuwa tayari amejiandaa na mahari ya shilingi za kitanzania milioni 100.

Ommy Dimpoz amzawadi Marioo
Ommy Dimpoz amzawadi Marioo
Image: Instagram

Msanii wa muda mrefu wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz ametangaza kumpa mwenzake Marioo zawadi ya shiingi milioni 5 pesa za kitanzania baada ya kufanikiwa kuwa mtu wa kwanza kumpaisha muigizaji mkongwe, Frida Kajala Masanja cheo kutoka kwa mama hadi bibi.

Akizungumza wakati wa hafla ya Marioo na Paula kusherehekea safari yao ya ujauzito, Dimpoz ambaye alikuwa mmoja wa wageni waalikwa katika hafla hiyo ya mwishoni mwa wiki jana alimpongeza Marioo kwa kumpa mimba Paula na kusema kwamba hatua hiyo moja kwa moja inamfanya Kajala kuwa bibi kwa mwanao mtarajiwa.

Dimpoz alisema kwamba Marioo ndio kijana wa kwanza kufanya udhubutu wa kumfanya Kajala kutarajia mjukuu hivi karibuni.

“Lakini pia Bwana Omari [Marioo], mimi nakusifu sana unajua. Wewe mtoto kiboko, kwa sababu wewe ndio umekuwa Mtanzania wa kwanza kumfanya Kajala aitwe bibi. Sio mchezo ujue. Ukiachana na hilo pia ukamfanya P Funk Majani aitwe babu. Ndio hivyo tena limekuwa jambo la heri. Kutokana na hicho ulichokifanya, cha kumfanya Kajala tumuite bibi, mimi nakupa zawadi ya milioni 5,” Ommy Dimpoz alisema.

Marioo na Paula wamekuwa kwenye mahusiano kwa kipindi cha takribani mwaka mmoja na siku chache zilizopita, waliweka wazi kwamba wanatarajia mtoto wao wa kwanza pamoja.

Marioo alianza kuchumbiana na Paula baada ya mrembo huyo kukatisha uhusiano wake na msanii Rayvanny.

Iliarifiwa kwamba Marioo alikuwa tayari amejiandaa na mahari ya shilingi za kitanzania milioni 100.