Mwigizaji Kate Actress afurahia baada ya kualikwa White House

NI moja kati ya wale ambao watahudhuria 'State Dinner' katika Ikilu ya White House na katika studio za Tyler Perry huko Atlanta katika taifa hilo la Marekani.

Muhtasari

• Atapata fursa ya kukutana na Rais wa Marekani Joe Biden na kuungana na Rais William Ruto.

Kate Actress.
Kate Actress.
Image: Instagram

Mwigizaji Kate Actress  ni mwenye furaha baada ya kupokea mwaliko wa chajio katika Ikulu ya White House ya Marekani.

Akieleza  habari hiyo ya kusisimua katika chapisho la mtandao wa kijamii alimpongeza balozi wa Marekani nchini Kenya Meg Whitman ambaye alimpa mwaliko huo.

"Habari za asubuhi. Msichana huyu wa kijijini atahudhuria STATE DINNER katika White House & a Luncheon katika studio za Tyler Perry huko Atlanta kwa mwaliko kutoka kwa Her Excellency Meg Whitman,” mama huyo wa watoto wawili aliandika.

Mwigizaji Kate alithibitisha tena kwamba kujumuishwa kwake kulikuwa faida nzuri kwa tasnia ya ubunifu ya Kenya.

Atapata fursa ya kukutana na Rais wa Marekani Joe Biden na kuungana na Rais William Ruto.

Eddie Butita ni mbunifu mwingine ambaye atakuwa Marekani kwani aliambatana na raisi Ruto katika ziara yake.

Akitumia mitandao ya kijamii, Butita aliunga mkono maoni ya Mwigizaji Kate, akikiri kuwa hii ilikuwa hatua kubwa kwa wabunifu wa Kenya kusikika kwenye jukwaa la kimataifa.