Desagu afichua mapato yake kutoka kwa youTube

"Kiwango cha juu zaidi kwa mwezi ni 400,000 ksh." Desagu alifichua

Muhtasari

•"Kiwango cha juu zaidi kwa mwezi ni 400,000 ksh." Desagu alifichua.

•Watu wengine hawajui vile YouTube hua inalipa. Kwa sababu saa zingine inatengemea urefu wa  video,umefanya video ngapi na pia watu wangapi wametazama.

Mchekeshaji Henry DeSagu
Mchekeshaji Henry DeSagu
Image: Facebook

Henry Desagu, almaarufu Prince of Mwihoko amefichua kiasi cha juu zaidi alichowahi kutengeneza kutoka kwa chaneli yake ya YouTube.

 

Akizungumza wakati wa mahojiano na Obinna TV, Desagu alisema  kiasi hicho ni ksh 400,000.

"Kiwango cha juu zaidi kwa mwezi ni 400,000 ksh." Desagu alifichua.

Aliendelea kufafanua jinsi YouTube wanavyolipa, akisema kuna mikakati ambayo YouTube hutumia kulipa, na haifanyi kazi tu na idadi ya views ambazo video ina, ambao ni mlinganisho wa wengi, akisema wanafuata urefu wa video. iliyochapishwa, muda wa kutazama, na idadi ya video.

 

“Watu wengine hawajui vile YouTube hua inalipa. Kwa sababu saa zingine inatengemea urefu wa  video,umefanya video ngapi na pia watu wangapi wametazama na pia kuna wakati unaambiwa vile mtu akiwa Kenya si vile yeye yuko nje ya Kenya analipwa.”

Hata hivyo, alisema njia yake kuu ya kupata mapato ni kupitia matangazo  na hategemei YouTube kabisa.

Akizungumzia jinsi alivyoifanya YouTube channel yake kukua, alisema alikuwa akiitangaza chaneli yake kwa kuiweka kwenye mitandao yake yote ya kijamii  na kuwaomba mashabiki na wananchi ku-subscribe, angalau katika kila post anayochapisha.

Alieleza jinsi ubunifu wake ulikuwa ukitaja sana mambo ambayo ni ya kawaida katika  jamii.

"Tulikuwa tukifanya maandishi madogo ili kuendana na Desagu, kisha tukaunda mhusika anayeitwa Desagu, ambaye alikuwa jamaa anagrow Mwihoko hajaoa na hana kazi ya kudumu na kimsingi kuhusu mapambano ya kile tunachopitia, kila siku." Desagu alishiriki tukio.