Willy Paul atazamia kufanya kolabo na Wizkid, Davido, Burna Boy na Chris Brown miaka 2 ijayo

Itaumbukwa katika albamu yake ya Beyond Gifted, msanii huyo aliwapiga nje wasanii wa Kenya na hakumshirikisha Mkenya hata mmoja kwenye albamu hiyo ya ngoza Zaidi ya 10.

Muhtasari

• Msanii huyo alimtaja msanii kutoka Marekani Chris Brown kuwa miongoni mwa wasanii anaolenga kufanikisha kolabo nao miaka miwili ijayo.

Willy Paul, msanii wa Kenya anayezidi kung’aa katika anga za muziki haswa baada ya kuachia albamu yake ya Beyond Gifted takribani mwezi mmoja uliopita ameweka wazi kuhusu malengo yake katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Willy Paul anasema kwamba lengo lake kuu katika kipindi cha miaka miwili ijayo si kustaafu muziki bali ni kuhakikisha amepaisha muziki wa Kenya kwenda kwenye majukwaa ya kitaifa.

Ili kufanikisha hilo, Pozee alisema kwamab analenga kufanikisha kufanya kolabo na baadhi ya wasanii wakubwa katika muziki wa kizazi kipya ulimwenguni.

Msanii huyo alimtaja msanii kutoka Marekani Chris Brown kuwa miongoni mwa wasanii anaolenga kufanikisha kolabo nao miaka miwili ijayo.

Kando na Brown, Willy Paul pia aliwataja mibabe wa muziki wa Afrobeats, Burna Boy, Wizkid na Davido kama wasanii anaolenga kufanya kolabo nao katika kipindi hicho cha miaka miwili.

“King Pozee, ninatazamia mambo makubwa katika miaka miwili ijayo, Chris Brown, Burna Boy, Davido na Wizkid, ndio wasanii ambao ninatazamia kufanya kolabo nao. Amini katika hatua ndogo ndogo, kijana wenu yuko tayari kuwafanya mjihisi kujivunia,” Willy Paul aliandika kwenye chapisho lake.

Itaumbukwa katika albamu yake ya Beyond Gifted, msanii huyo aliwapiga nje wasanii wa Kenya na hakumshirikisha Mkenya hata mmoja kwenye albamu hiyo ya ngoza Zaidi ya 10.

Akijibu hilo, Pozee alisema kwamba alichagua kutowashirikisha wasanii wa Kenya kwa kile alihisi wengi wao hawana cha mno kuchangia kwenye muziki isipokuwa chuki tu.