Justina Syokau amuomba ndoa Mhubiri Kanyari

Justina Syokau anasema kuwa anatafuta mwanamume kama Kanyari sababu ni mwanamume mzuri

Muhtasari

•Syokau amewashangaza wengi baada ya kumuomba ndoa mchungaji Victor Kanyari wa Salvation Healing and Ministry.

•Pia aliongeza kuwa wanawake wanahitaji kuolewa na wanaume ambao wanalinda watoto wao.

JUSTINA SYOKAU
JUSTINA SYOKAU
Image: Facebook

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Justina Syokau amewashangaza wengi baada ya kumuomba ndoa mchungaji Victor Kanyari wa Salvation Healing and Ministry.

Katika video inayosambaa mtandaoni, Justina alienda kwa madhabahu, kupiga magoti na kumuuliza Kanyari kama atamuoa.

Utanioa? Uko na kitu ya kuambia watu?”

Kanyari alicheka huku Syokau akiendelea na kumsifu mchungaji huyo kuwa mwanamume mzuri na kukiri kuwa anatafuta mwanamume kama yeye. 

Alisema kuwa Kanyari amekuwa mfano kwani akipeleka wanawe out huwa wanahisi vizuri na kuomba Mungu kupata bwana kama yeye.

Kuna kitu moja nimeona, huyu mchungaji ni mzuri wacheni niwaambie, natafuta mwanamume kama huyu. Mwanamume mwenye anapeleka watoto wake outing, mwanamume mwenye anahakikisha watoto wake wanasomea USA, mwanaume ambaye analida watoto...Hujui chenye unafanya, wakati unapeleka akina Sky out tunaskia vizuri tunasema Mungu tunaomba bwana kama huyu...Wewe mchungaji umekuwa mfano,"

Justina alisema kuwa hajawai ona mwanawe amepelekwa out na kwamba hamjui babake. Pia aliongeza kuwa wanawake wanahitaji kuolewa na wanaume ambao wanalinda watoto wao.

Mimi kama single mother sijwai ona mtoto wangu amepelekwa out hata hajui baba yake...Tunahitaji kuolewana wanaume ambao wanalinda watoto wao...,"