Daah! ''Alinipa sh100 baada ya kulala kwake usiku wote'' Mwanamke alia

Malimwengu haya! Wanawake wa mumu humu kenya walifunguka waziwazi na kusema kuwa, wanaume wa humu kenya ndio waume wenye mkono birika si kidogo.

Zaidi ya hayo, asilimia kubwa ya wanawake walisema kuwa wako radhi wafe kuliko kutumia pesa nyingi sana kwa mwanaume.

Mwanamke mmoja alifunguka kwenye mtandao wa kijamii na kusimulia hadithi yake na jamaa mmoja aliyekuwa mpenzi wake.

Binti huyu alisema kuwa alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mmoja ambaye alimpa shillingi 100 baada ya kulala kwake usiku mzima.

Rachael alisema,

''Nilikuwa na mchumba na siku ya kwanza baada ya kulala kwake, nlimuomba bwana huyu hela kwani sikuwa na kazi.

Amini usiamini, jamaa huyu alinipa shilingi 100. Nilikasirika sana kwani niliona ni kama bwana huyu ananaidharau sana na nkamwambia awache pesa hizo juu ya meza na alipo enda kazini, sikumtafuta tena. Hiyo siku ilikuwa siku ya mwisho kuona huyo mwanaume.''

Zaidi ya hayo, Rachael alisema kuwa, iwapo jamaa huyu angemuoa, basi angekuwa maskini maisha yake yote na hivyo basi, anashukuru kuwa hakuendelea na uhusiano huo.

Vile vile, Rachael alisema kuwa, alipata funzo kali na kuapa hakuna siku ata moja atamuomba mwanaume pesa.
Hivyo basi, Rachael alitafuta kazi na kwa miaka saba, alifanya kazi na kutafuta pesa zake mwenyewe mpaka ile siku ambayo ataolewa.

Kwa sasa, Rachael ameolea na alisema kuwa mume wake humpa pesa ata kabla hajaomba pesa zile.
''Mume wangu ndio mtoa huduma na huwa ananipa pesa kila mwezi kabla hata sijaomba pesa zile.'' Rachael alisema.
Licha ya hayo, mwanamke mwengine alifunguka na kusema kuwa, ameolewa kwa miaka 25 sasa na hakuna siku hata moja ambayo mume wake amempa hela.
Sadiki usisadiki, mwanamke huyu alisema kuwa, mume wake hulipwa mshahara mara nne zaidi ya pato lake na hakuna siku ata wakienda dukani mume wake amemnunulia kitamba cha hedhi ( sanitary towels).
Mwanamke huyu alizidi kusema imefika wakati ambao anaeza sema wazi kuwa, amechoka na maisha yale.
Licha ya hayo, mwanamke huyu alisema kuwa, hakuna siku mume wake amenunua maziwa au mkate anaporudi nyumbani na bado atakunywa kiamsha kinya, ale chakula cha saa sita na chajio.
Je ni shilingi ngapi ambazo mpenzi wako amewahi kupa?