Dakika 5 tu niage dunia, Msanii wa nyimbo za injili Roz Haki afunguka

Screenshot_from_2019_12_02_15_42_52__1575292319_37228
Screenshot_from_2019_12_02_15_42_52__1575292319_37228
Msanii wa nyimbo za injili Roz Haki amefunguka jinsi amebadilika na kuwa chombo cha kumtukuza Mungu.

Hii ni baada ya kupitia hali ngumu ya maisha pamoja na kusongwa na mawazo.

Roz Haki alikuwa katika kitengo "cha ilikuwa aje", kipindi cha Bustani la Massawe.

Kilichomsumbua hapo awali ni makovu ya kubakwa na idadi ya watu asiowafahamu sehemu ya burudani ya eneo la Lang'ata viunga vya jiji kuu la Nairobi.

Tazama video yake hapa:

“Niliporudi na kurudi kunywa nikawa nahisi kulegea. Rafiki yangu akanionyesha sehemu ya kutulia. Nilikuwa naskia uchungu sana kwa kichwa. Mwanaume akaingia nikama anavuta mlango na akanichapa nikaanguka. Niliamka asubuhi nakuta watu wawili kwa nyumba na sikujua kilichofanyika…” Roz alisimulia.

Roz hatimaye alijitua vitendo vyake vya kutoroka wazazi na kuishi na marafiki wabaya mtaa wa Kibera.

"Mpaka leo sina habari idadi ya watu walionibaka. Nilipopata fahamu kulikuwa na watu karibu walionipa nauli huku wakisema sisi hata tumekuja saa hii. Wakati huo nilikuwa nalia na kujuta sana. Singeweza kupanda gari..." Roz.

"Nilienda hospitali nikatibiwa ila nikabaki na mawazo tele. Sikupata ugonjwa na hapo nikarudi Kibera. Marafiki zangu waliniona wakashtuka nikajua kuna kitu wanafahamu..." Roz.

Roz aliona safari yake ya kufanya sanaa ilikuwa tayari ishapata mkosi.

"Nikawa najilaumu pengine kuna kitu ningefanya kuzuia. Kidogo nikaanza kunywa pombe kwa mwezi ili nisahau. Nikaona suluhisho ni kujitia kitanzi..."

Roz alitamani kujiua.

 "Kuna ile unahisi hauna thamani...mama alishtuka kama naweza weka mambo kama hayo kwa muda mrefu..."

"Msamaria alinipata kabla nijue. Nilikuwa nishaandika will na baadaye nikajikuta kwa ICU. Madaktari wakasema nilikuwa nabakisha dakika 5 nife..."

Roz kwa sasa amebadilika na anafanya kampeni za kuhamasisha vijana.

"Nilikuwa nimekunywa tu sumu. Kwa hayo yote mungu amefanya makovu yangu yakawa nyota.

"Hapo sasa nikafungua taasisi yangu ya kuwapa wasichana na vijana motisha. Haijalishi unayopitia unaweza ukabadilika..." Roz alisema.

Mhariri: Davis Ojiambo.