Githri man

Easy Come Easy Go: ‘Githeri man’ arejelea hali yake ya uchochole.

  Martin Kamotho  alias Githeri man  alijipa umaarufu wakati wa uchaguzi mkuu wa 2017 alipopigwa picha akiwa kwenye foleni ya kupiga kura  huku mkononi akijihami kwa mfuko wa plastiki uliokuwa na chakula chake –Githeri .Hakutaka kufanya kimoja kabla ya kurejelea kingine na ‘busara’yake hiyo ikamletea mazuri .Kando na kuangaziwa pakubwa na vyombo vya habari ,baadaye Kamotho alizawadiwa na watu binafsi na hata kusifiwa na  wengine .

Must Read: Still Single?Sababu 8 zinazokufanya usiwe na Mpenzi

Maisha yake ya umaskini yalionekana kumwaga  kwa sababu  alialikwa kwenda Ikulu  kupokea tuzo ya Head of State Commendation (HSC),  na pia akatunukiwa shilingi laki moja .

Awali kabla ya umaarufu wake alikuwa pia na tatizo la kunywa pombe na mambo yalionekana kubadilika huku wengi wakitaraji angeuitumia fursa hiyo kubadilika na kujiboresha . Kampuni kadhaa zilimtumia  ili kuangaziwa kwa kutoa ahadi ambazo nyingi hazijatimizwa .Kamotho anasema kwa jumla alipewa shilingi 150,000 lakini pesa  hizo zimemfanya hata kuwa maskini zaidi kwani hakuna aliyetoa suluhisho la kudumu kumnasua kutoka umaskini .

‘Makena Cheater’:  Gari La Makena lachafuliwa kwa maandishi kwa  madai ya penzi la pembeni 

Baadaye kwa ajili ya uraibu wa kunywa pombe alijipata katika kituo cha kumsaidia aache ulevi cha Mama Care Rehabilitation Centre, Kiambu. Rais  Uhuru Kenyatta alihudhuria hafla hiyo ambapo Kamotho na wengine 77 walihitimu .Lakini cha kuvunja moyo sasa ni picha inayosambazwa  mtandaoni akiwa anakokotwa katika toroli ,akionekana kuwa mlevi . Huenda jamii haikumsaidia Githeri man kwa kumpa  alichohitaji au  labda hajapata busara ya kuamua kujisaidia mwenyewe .

 

 

 

Photo Credits: Hisani

Read More:

Comments

comments