Familia Maskini Yaomba Usaidizi Wa Karo Wa Kijana Kipofu Aliye Na Ndoto Ya Kuwa Wakili

kipofu
kipofu
Familia moja kutoka kijiji cha Mungachi wadi ya Sitikho eneo bunge la Webuye magharibi inatoa wito kwa wahisani wema kuingilia kati na kumsadia mwanao ambaye ni kipofu kulipa karo na kutimiza ndoto yake ya kuwa wakili.

Austime Lusweti ambaye ni mwanawe mama mmoja aliyegonga vichwa vya habari kwa kujifungua watoto wanne mwaka wa 2014 alipata alama ya 313 kwa mtihani wa KCPE wa mwaka jana na kuitwa katika shule ya kitaifa ya Thika na bado hajajiunga kutokana na umaskini wa hali ya juu.

Mamake Easther Lusweti ametoa wito kwa serikali ya kaunti, viongozi pamoja na wahisani wema kuingilia kati na kuwapa usaidizi ili mwanao apatae masomo yake ili aweze kuwasadia pamoja na wanao siku za usoni.