Familia: Raila hatorejea nyumbani hivi karibuni

Familia ya kiongozi wa  Upinzani Raila Odinga  imefunguka kuhusu anachoogua kiongozi huyo wa chama cha ODM  ambaye anaendelea kupata nafuu  huko mashariki ya kati .

Mkewe Ida Odinga,kakake mkubwa   Oburu Odinga na dadake mdogo Ruth Odinga  wamesema kwamba Raila hayupo hatarini lakini hatarejea nchini hivi karibuni .

Ida  Ida amesema mume wake alitibiwa tatizo la neva  lilikuwa likimpa shida katika mguu wake mmoja  na anahitaji muda zaidi wa kupumzika . Kwa ajili ya matibabu aliyopokea atasalia UAE  hadi atakapoweza kurejelea shughuli za kisiasa .

Familia hiyo imeeleza kufadhaika na habari zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zikieleza maradhi   ambayo Raila anadaiwa kuugua .

Ida amesema habari kama hizo zinafaa kupuuzwa na wakenya kama uvumi na amewashukuru wakenya wenye nia njema ambao  wamekuwa wakimuombea Raila afueni ya haraka.

Ida alisema bwana Odinga yupo katika hospitali moja inayoendeshwa na wajerumani ,Dubai .

Ilikuwa  mara ya kwanza kwa Ida kufunguka kuhusu tatizo la afya la mumewe  huku akiongeza kwamba amekuwa akizungumza naye karibu ‘kila saa au baada ya saa mbili’