Familia yaomba kusaidiwa kupata wapendwa wao waliozama

Familia moja kutoka kijiji cha mwembula wadi ya sitikho kwenye eneo bunge la webuye magharibi imetoa wito kwa serikali kuingilia kati na kuisaidia kupata miili ya baba na mwanawe walioanguka majini mwezi mmoja uliopita.

Baba na mwanawe walianguka majini tarehe ishirini na moja mwezi wa kumi na mbili mwaka jana kutokana na mzozo wa ndoa ambapo mkewe wa kwanza wa marehemu waliyekua wamezozana kwa muda kurejeshwa kwa lazima na mwanawe ndiye aliyetoa ufungua wa nyumba kinyume na babake ambaye alijaribu kumfukuza na kijana akaelekea mto Nzoia na kuanguka majini kisa kilichomlazimu babake kumuokoa lakini pia akazidiwa na maji na hadi sasa miili hiyo haijapataikana licha ya kutafutwa.

Hata hivyo mke huyo alidinda kuongelea swala hilo na pamoja na mkemwenza wakataka serikali kuwasaidia kupata miili hiyo.

Aidha wazazi, na wakazi wa eneo hilo wamelalamika kuwa hakuna mtu kiongozi wa serikali aliyefika kuwafariji na kutaka wafanye hima na kusaidia kupata miili hiyo kwani familia inapitia wakati mgumu.