PATANISHO: Nashuku boss wangu mwanajeshi ana uhusiano na mke wangu

Ken anayefanya kazi na kitengo cha wanajeshi alituma ujumbe akiomba usaidizi akidai kuwa huenda bosi wake anakula uroda na mke wake na anasema amechoshwa na anakadiria kumuua jamaa huyo.
"Hii ni kitu ilianza mwaka uliopita kwani nilipata ujumbe wa simu kutoka kwa boss wangu kwa simu yake na sikumuuliza. Juzi tulienda Somalia mwezi wa nane na familia yangu ilikuwa holiday Nairobi." Ken alisema.

Aliongeza,

Kijana wangu nilikuwa nimemnunulia simu na nikamwambia anieleze jinsi vitu vilivyo. Kutumanishia mke wangu vitu huyo jamaa akamuomba mke wangu nambari ya simu. Juzi tulikuwa na sherehe kabarak na familia yangu ilipofika kijana wangu akanionesha picha walizopiga na boss wangu."

Ken anasema baada ya mda mchache mke wake alihama na alipoenda kumuuliza boss wake kuhusu zile picha, boss alisema kuwa walikuwa marafiki na hiyo siku walipiga picha katika sherehe.

Jamaa anasema kuwa anapitia machungu kweli kwani kama mwanajeshi anaenda kazini lakini mkewe anaeneza mahusiano na boss wake.

Hata hivyo juhudi zetu za kumfikia mkewe Ken hazikufua dafu na ilibidi tuwape wanajambo fursa wamshauri jamaa huyu.