Uganda yatangaza visa 30 vipya vya maambukizi ya corona

Wizara ya afya nchini Uganda imetangaza visa vipya 30 vya maambukizi ya ugonjwa wa corona katika sampuli 3,758 zilizopimwa jana jumapili. Visa hivyo vinafanya idadi ya maambukizi kufikia 646 nchini humo.

Kufikia sasa wafanyakazi wa afya walioambukizwa virusi hivyo nchini Uganda imefaikia 22 baada ya maafisa wengine wa afya wanne kudhibitishwa kuwa na virusi hivyo,.